Yanga inajiunga na Simba katika kombe la mabingwa Afrika

anzania itawakilishwa na timu nne za soka katika mashindano ya michuano ya Caf mwakani.

Hatua hiyo inajiri baada ya taifa la Tanzania kuorodheshwa miongoni mwa mataifa 12 barani Afrika yenye ligi bora .

Hiyo inamaanisha kwamba klabu ya Yanga ambayo ilimaliza katika nafsi ya pili itajiunga na mabingwa wa ligi ya Tanzania Simba katika kushiriki ligi ya mabingwa.

Timu nyengine zitakazowakilisha Tanzania katika michuano hiyo ya Caf ni Azam Fc na KMC zitakazoshiriki katika kombe la Shirikisho.

KMC itashiriki katika kombe la Shirikisho kwa mujibu wa kanuni hiyo ambayo inasema kuwa timu iliomaliza katika nafasi ya tatu ndio mabingwa wa kombe la FA , hivyobasi mshindi wa 4 atapata nafasi ya kucheza kombe la shirikisho kwa sababu bingwa wa FA ataiwakilisha nchi katika mashindano hayo.

Azam FC ni mabingwa wa kombe la FA

Rais wa TFF Wallace Karia amezitaka klabu zilizopata nafasi kusajili kwa umakini ili kujiandaa kwa mashindano ya CAF kwa lengo la kutopoteza nafasi ya kuingiza timu nne katika mashindano ya CAF.

Tayari CAF imefungua dirisha kwa mashirikisho kusajili timu zao.

CAF imesema kuwa mwisho wa usajili wa timu hizo kushiriki ni mwezi Juni 30,2019

Baadhi ya mataifa ambayo yameorodheshwa kuwa na ligi bora Afrika ni pamoja na Algeria, Angola, DR Congo, Misri , Guinea, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini,Sudan Tunisia na Zambia.

CHANZO: BBC

error: Content is protected !!