Wimbo wa Takataka wapigwa marufuku Kenya

Ezekiel Mutua ( kulia) amesema Takataka umeimbwa kwa lugha katili na unawafanya wanawake kuonekana kama vifaa na kuhimiza wanaume wawaumize

Mamlaka nchini Kenya zimepiga marufuku kuchezwa kwa wimbo Takataka, unaosemwa kuwa unawatusi wanawake.

Bodi ya kudhibiti filamu nchini Kenya imezuwia mara moja wimbo Takataka- ulioimbwa na msanii Alvin almaarufu Alvindo uliozalishwa na kampuni ya FastCash Music Group.

Mkurugenzi wa Bodi ya udhibiti wa viwango vya filamu nchini Ezekiel Mutua aliuelezea wimbo huo kama wenye wakishamba na wenye matusi na kuongeza kuwa ” kama watu wanaowajibika hatuwezi kuukubali .”

” Wimbo Takataka umeimbwa kwa lugha katili unaowafanya wanawake kuwa kama vifaa na kuhimiza wanaume waumizwe kuumizwa na wanaume ,” alisema bwana Mutua katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za mamlaka hiyo mjini Jumanne.

Pia alisema kiuwa ni jambo la kuhofia kuwa kwanza wimbo huo haukuwasilishwa kwenye mamlaka hiyo ili uweze kukubaliwa.

“Kuanzia leo, wimbo Takataka haupaswi kuchezwa mbele ya hadhira wala kwenye chombo chochote cha utangazaji eneo lolote katika jamuhuri ya Kenya. Hakuna Dj anayepaswa kucheza iwe katika kiytuo cha utangazaji au katika burudani yoyote ,” ilieleza sehemu ya taarifa.

Bodi hiyo imesema kuwa kumekuw ana vifo vingi vya wapenzi katika siku za hivi karibuni na muziki wa aina hiyo na ujumbe uliomo unachochea aina hii ya uhalifu.

Mutua aliviomba vyombo vya habari kuwa na ushirikiano na Wakenya katika kuzuwia miziki ya aina hiyo kulingana na mtazamo wao.

“Baadhi ya wasanii huimba miziki ya aina hiyo ili wasikike kama watu wenye utata na kupata ufuasi ambao wanautumia kutengeneza pesa ,” alieleza na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na kukua kwa utamaduni wa kishetani.

matokeo yake, Alvin ameitwa na Bodi hiyo na amepewa muda wa wiki mbili wa kujiwasilishana iwapo atashindwa kufanya hijvyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Msanii huyo pia anakabiliwa na hatari kunyang’anywa kibali cha uanachama wa Mamlaka nyingine za udhibiti wa maudhui ya Muziki ikiwemo Mahalaka ya haki miliki ya Muziki nchini Kenya na Chama cha Wazalishaji wa mziki nchini Kenya.

Licha ya kucheza muziki huo moja kwa moja mbele ya hadhira , TV na redio, wimbo Takataka pia hautachezwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Bodi imeagiza kuondolewa kwa wimbo huo kwenye tovuti zote ,” imesema taarifa yake.

Akielezea ni kwanini iliichukua mamlaka hiyo miezi minne kuchukua hatua dhidi ya wimbo Takataka uliotolewa mwezi Januari mwaka huu, Bwana Mutua alisema kuwa Bodi ilikuwa makini ili kufuata mchakato unaokubalika kisheria na ushahidi wa kutosha wa kesi dhidi ya maudhui ya wimbo huo.

Bodi hiyo imewataka wasanii na mashirika ya habari kubuni na kutangaza ujumbe unaojenga jamii.

” Usanii ni kioo cha jamii, lakini usanii lazima uweke mwongozo sahihi kuhakikisha ujumbe wanaoutoa unaimarisha maadili mema wakati wote,” ilieleza taarifahiyo na kuongeza kuwa utupu, unyanyasaji wa kijinsia na kuwashushia hadhi wanawake ni mambo ambayo hayapaswi kuonyeshwa kama ndio njia ya maisha.

Matukio ya mauaji ya wapenzi na unyanyasaji dhidi ya wanawake liliwemo tukio la mwanaume mmoja aliyemuua kwa panga mpenzi wake wa kike mchana katika eneo la Eldoret, yalilishitua taifa.

katika miaka ya ya hivi karibuni wanasanii katika mataifa ya nchi za Afrika mashariki wamekuwa wakikabiliwa na hatua za mamlaka husika na maudhui ya muziki na kuwekewa marufuku ya kazi zao.

Nchini Tanzania Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) liliwawafungia kazi zao wanamuziki nyota wa Bongo flava Diamond Platnumz na Rayvany baada ya kutumbuiza kibao kilichofungiwa: Mwezi Disemba wakati Basata ikiwaangushia rungu wasanii hao ilidai kuwa

Uamuzi wa Basata ulifuatia kitendo cha wasanii hao kutumbuiza jukwaani kibao kilichopigwa marufuku na mamlaka cha Mwanza.

error: Content is protected !!