Waziri mkuu wa Malesia, amesema nchi yake inayo haki ya kumlinda na kutomrudisha India mwanazuoni wa kiislamu mwenye asili ya India dkt Zakir Naik

Mahathir Muhammed, waziri mkuu wa Malesia amesema kwamba nchi yake inayo haki ya kumlinda na kutomrudisha India  Dokta Zakir Naik.

Waziri mkuu Mahathir alikuwa akizungumza katika kipindi kimoja alichoshiriki kuhusiana na matakwa ya serikali ya India juu ya msomi wa dini ya kiislamu mwenye asili ya India anayeishi uhamishoni nchini Malesia, Dokta Zakir Naik. Serikali ya India inamtuhumu dokta naik kwa kufadhili ugaidi na utakatishaji fedha.

Mahathir alisema kabla serikali ya India kutuma ombi la kutaka Naik arudishwe ilipaswa kwanza imuhakikishie usalama wake kwani  dokta Zakir Naik mwenyewe anafikiri India haiwezi kumfanyia uadilifu katika kesi hiyo inayomkabili, ni kwa sababu hiyo Malesia ina haki ya kumlinda na kutomrudisha  India mwanazuoni huyo.

Dokta Naik ni moja ya wanafunzi wa mwanazuoni maarufu na mwanaharakati kutokea Afrika ya kusini ambaye alifariki mwaka 2005, Ahmed Didat. Naik anafahamika dunia nzima kutokana na makongamano na madarasa anayoyaendesha kupitia kituo chake cha runinga “Peace TV” na majukwaa mengine.

Naik ambaye ni bingwa wa historia na ulinganishaji wa madhehebu ya dini mbalimbali pia anafahamika kutokana na hotuba zake dhidi ya ugaidi.

error: Content is protected !!