Watumiaji wa simu janja waonywa kuwa makini na Mpinga Kristo

Patriarch Kirill

Askofu Mkuu Kirill akifanya ibada ya sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo

Tabia ya watu kutegemea sana simu janja (smart phone) pamoja na teknolojia ya kisasa kunaweza pelekea kuja kwa Mpinga Kristo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Orthodox la Urusi Askofu Kirill ameonya.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Urusi wamejibu ujumbe huo kwa ucheshi na kushuku huku baadhi wakilishutumu kanisa hilo kuwa “linautumikia utawala wa Rais Vladimir Putin.”

Akiwa anaongea na televisheni ya Taifa ya Urusi, Askofu Mkuu Kirill amesema watumiaji wa simu janja wanatakiwa kuwa makini wakiwa wanatumia programu mbali mbali za mtandao kwasababu zimewasilisha “fursa ya kudhibiti binadamu ulimwenguni”.

“Mpinga kristo ni mtu ambaye atakuwa ndio kichwa cha tovuti ulimwenguni akidhibiti binadamu,” amesema.

“Kila mara unapo tumia simu yako janja, bila kujali una penda au hupendi, umewasha progamu ya kuonyesha mahali ulipo au la, kuna mtu anaweza kugundua mahali ulipo, vitu unavyo penda na vitu unavyo viogopa,” Askofu Mkuu Kirill ameiambia Rossiya 1.

“Kama sio leo, basi ni njia za kesho na teknolojia yake itatokea kwamba itakuwa haikupi taarifa za aina zote pekee bali pia itakuwa inaruhusu matumizi ya taarifa zako.

“Je ushawahi kufikiria ni nguvu kiasi gani ambayo itajilimbikizia mikononi mwa wale wanaopata ujuzi kuhusu kile kinachoendelea duniani? Udhibiti huo kutoka sehemu moja unatueleza kuja kwa Mpinga Kristo.”

Askofu Kirill amesema Kanisa lake halikupinga “maendeleo ya kiteknolojia”, badala ya “maendeleo ya mfumo ambao una lengo la kudhibiti utambulisho wa mtu”.

Lakini si watumiaji wote wa mitandao ya kijamii walikubali kumwelewa.

“Kanisa halipo kinyume na maendeleo ya sayansi na teknolojia, lakini lina mashaka na uhuru wa mtu binafsi. Ndiyo, hakika,” mtumiaji mmoja wa

“Kanisa halipo kinyume na maendeleo ya sayansi na teknolojia, lakini lina mashaka na uhuru wa mtu binafsi. Ndiyo, hakika,” mtumiaji mmoja wa Twitter amesema.

“Tabasamu, Mpinga Kristo anakaribia kupaa,” mtu mwingine amendika katika mtandao wa Twitter, na kuambatanisha na picha ya mwanamke na Askofu Kirill na wawakilishi wengine wa kanisa.

Askofu Kirill yupo karibu na Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye hushiriki katika sherehe kubwa za Kanisa na amekwisha safiri kwenda Mlima Athos na maeneo mengine maarufu ya katika imani ya kikanisa. Mapadri wengi wa Urusi wanaelewa na kuikubali ajenda ya Rais Putin.

Wakati ambapo uhuru wa mtandao unazidi kuzuiwa nchini Urusi – na mamlaka inaripoti kuwa wanajaribu kuunda mtandao wa Kirusi wa kujitegemea – ukaribu huu umesababisha wengine kumshutumu Askofu Kirill kwa kuingiza sera za serikali katika mamlaka ya Mungu.

“Wamepiga marufuku mtandao wa kimataifa nchini Urusi ili Mpinga Kristo asije kutoka humo,” mtumiaji mmoja wa mtandao wa kijamii alisema.

Siku ya Jumamosi, Kanisa la Orthodox la Ukraine lilitengana na Kanisa la Kirusi kufuatia karne za uongozi wa Urusi, na kurasimisha uamuzi uliotangazwa mnamo mwezi Oktoba.

Hatua hiyo iliibua majibu ya hasira huko Moscow na kuimarisha mgawanyiko katika Kanisa la Orthodox kote duniani.

CHANZO: BBC

error: Content is protected !!