Watafiti kutoka Ureno wagundua Nyota inayofanana sana na Jua

Watafiti wa masuala ya Anga, wamegundua nyota inayofanana na Jua.

Wataalamu hao kutoka taasisi ya elimu ya unajimu na fizikia ya nchini Ureno wamegundua nyota “jamii ya Jua”. timu ya kimataifa kutoka taasisi hiyo ilikuwa ikifanya utafiti juu ya umri, chemikali zilizomo, na mienendo ya nyota elfu 17 katika galaksi ya Kilimia .

Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na watafiti hao kwa kutumia hadubini za rezolusheni za viwango vya juu waligundua nyota inayokadiriwa kuwa na umri wa miaka bilioni 4.5 ambayo wameilezea kama ndugu pacha wa Jua ambayo imepewa jina la HD186302 .

Nyota hio inasemekana ipo umbali wa miaka ya nuru (light years)  184 kutoka duniani. Matokeo ya utafiti huo muhimu yamechapishwa  katika jarida la “Astronomy and Astrophysics”.

error: Content is protected !!