Wachezaji wawili wa Ajax ambao ni waislamu raia wa Moroko wafungulia funga zao za Ramadhan wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham

Wachezaji wa soka wa timu ya Ajax, Mazraoui na Ziyech, ambao ni waislamu wafungulia funga zao za Ramadhan wakati wa mchezo wa ligi ya mbingwa dhidi ya Tottenham.

Ajax ambayo ilifika nusu fainali za ligi ha klabu bingwa Ulaya kwa kuzitoa Real Madrid na Juventus wameshinwa kutamba mbele ya Tottenham.

Mchezo huo ulichezwa katika dimba la Amsterdam Arena, Katika mchezo huo wachezaji wa Ajax ambao ni waislamu Noussair Mazraoui na Hakim Ziyech, walifungulia funga zao wakti mchezo ukiendelea.

Wachezaji hao wawili raia wa Moroko  walioingia na kikosi cha kwanza, ilipofika dk ya 21 ya mchezo walikwenda katika kona ya uwanja na kufungulia huku kamera za warusha matangazo zikiwamulika.

Kwa upande mwingine goli la 2 la Ajax liliwekwa kimiani na Hakim Ziyech mnamo dk 35.

error: Content is protected !!