Wachezaji bora wa kutizamwa kombe la dunia la wanawake

Ni wachezaji gani watang’ara katika kombe la dunia la wanawake? Nani ataibuka kama nyota kwenye michuano hiyo.

Lieke Martens (Uholanzi)

Nyota huyu wa Uholanzi alisaidia nchi yake kushinda michuano ya Ulaya miaka 2 iliyopita. Martens tayari ni miongoni mwa wachezaji bora ulimwenguni. Ana miaka 26 na anakipiga klabu ya Barcelona, amepachikwa jina la “dada mdogo wa Messi” kwasababu ya aina yake ya uchezaji. Bingwa wa chenga, mmaliziaji mzuri na 2017 alitangazwa na FIFA kuwa mchezaji bora wa kike upande wa wanawake.

Christine Sinclair (Canada)

Mchezaji wa bora kuliko wa Canada na mfungaji anayeongoza. Hii ni michuano yake ya tano ya kombe la dunia inayofanyika Ufaransa. Licha ya kuwa na miaka 36, Sinclair ni mchezaji wa kutumainiwa katika timu. Tangu alipoanza kusakata kabumbu akiwa na miaka 19, Sinclair amecheza mechi 282 na kufunga mabao 181 kwa ajili ya nchi yake.

Wendie Renard (Ufaransa)

Wendie Renard (kushoto) ni tegemeo la klabu ya Olympique Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa. Beki huyo wa kati ameshinda ligi ya Ufaransa na klabu ya Lyon kwa mara 13 mfululizo, na mashindano ya klabu nibgwa Ulaya mara sita. Renard ni mmoja ya washambuliaji mahiri duniani na atakuwa tegemeo kwa Ufaransa wakijaribu kushinda taji hilo nyumbani.

Lucy Bronze (England)

Lucy Bronze ni moja ya wacheza soka bora duniani na bila shaka atakuwa tegemeo kubwa kwa timu yake ya England. Bronze ambaye jina lake kamili ni Lucia Roberta Tough “Lucy”, ameshinda tuzo nyingi ngazi ya vilabu. Kwa England, alimaliza nafasi ya tatu kombe la dunia la 2015 na nusu fainali michuano ya Ulaya ya 2017. Mwaka huu, mshambuliaji huyo katika klabu ya lyon anatarajiwa kung’ara Zaidi.

Irene Paredes (Uhispania)

Mwenye kasi, imara katika kutafuta mipira na udhibiti wa mipira ya juu, Paredes ni nguvu ya kutegemewa. Beki huyu wa kati ambaye ameichezea PSG tangu mwaka 2016, ni kiungo eneo la mbele. Paredes aliifungia Uhispania goli 4 wakati wa hatua za kufuzu kombe la dunia na kumfanya kuwa kinara wa magoli kwa timu yake. Paredes ni mshambuliaji wa juu na atakabiliana na Ujerumani hatua ya makundi.

Marta (Brazil)

Pambana dhidi ya ubaguzi, kutoungwa mkono, dhidi ya kila mmoja anayesema huwezi fanya”, Marta Vieira da Silva aliandika katika jukwaa la wachezaji. Ana miaka 33 na ameshinda tuzo ya mchezaji bora mara 6. Kwa wengi, mshambuliaji huyu wa Brazil anayekipiga klabu ya Orlando Pride bado ni moja ya wachezaji bora wa dunia. Pasi na shaka, huyu ni miongoni mwa wachezaji wakongwe kwenye soka la wanawake.

Rio 2016 Frauenfussball USA Carli Lloyd (Getty Images/P. Vilela)
Carli Lloyd (Marekani)

Mshambuliaji huyo pengine ni miongoni mwa wachezaji walio na shinikizo duniani. Alifunga magoli yaliyoipatia Marekani media ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki ya 2008 na 2012. Fainali zilizopita za kombe la dunia 2015, alifunga hat trick dhidi ya Japan. Mechi 273, magoli 110 na assist 52. Mwaka 2015 na 2016 alikuwa mchezaji bora wa mwaka.

Asisat Oshoala (Getty Images/AFP/A. Kisbenedek)
Asisat Oshoala (Nigeria)

Kipaji cha Oshoala kilichomoza mwaka 2014 wakati wa michuano ya kombe la dunia chini ya maka 20. Oshoala alipoteza fainali lakini aliibuka na mpira wa dhahabu kama mchezaji bora na kiatu cha dhahabu kama mfungaji bora. Hivi sasa anakipiga klabu ya Barcelona. Ameshinda mara mbili michuano ya kombe la Afrika na kutangazwa mchezaji bora wa kike upande wa Afrika mara tatu.

Deutschland - Tschechische Republik, Frauen WM-Quali Dzsenifer Marozsan (picture-alliance/GES/T. Eisenhuth)
Dzsenifer Marozsan (Ujerumani)

Ana chenga, hatari akiwa eneo la mbele na mzuri sana. Marozsan ni moja ya wachezaji walio na mbinu Ujerumani. Ana miaka 27 na ameshinda UEFA mara 4. Mwaka 2013 alishinda Ulaya na mika mitatu baadae alishinda medali ya dhahabu. Hivi sasa Marozsan anataka kuiwezesha Ujerumani kushinda kombe la dunia.

Fußball Frauen - VFL Wolfsburg vs Olympique Lyon (Reuters/V. Ogirenko)
Amandine Henry (Ufaransa)

Angalau kila hatua ya ushmabuliaji lazima mipira ipitie kwa Amandine Henry (kulia.), bila kujali anachezea klabu yake ya Olympique Lyon au timu ya taifa ya Ufaransa. Ana mbinu za kuumiliki mpira na kupenya katika safu ya ulinzi. Namna mchezaji huyo anavyousoma mchezo ni mojawapo ya kigezo kinachomfanya kuwa mchezaji bora duniani.

League Semi Final - Melbourne v Perth: Samantha Kerr macth einen Salto (Getty Images/G. Denholm)
Samantha Kerr (Australia)

Samantha Kerr anashikilia rekodi ya kufunga magoli 50 katika ligi ya taifa ya wanawake Marekani. Akiwa na miaka 15 alianza kuichezea timu ya taifa ya wanawake ya Australia. Tangu wakati huo ameiongoza “Matildas” kupanda hadi nafasi ya 6 katika viwango vya FIFA. Huwa anasherehekea kila goli kwa kuruka samasoti, tukio linalosubiriwa na mashabiki zake.

Italien Champions-League-Finale der Frauen Wolfsburg vs. Lyon in Reggio (Getty Images/AFP/G. Cacace)
Saki Kumagai (Japan)

Kumagai ameshinda ligi ya Ufaransa na klabu ya Olympique Lyon, mara sita na UEFA mara nne. Kama nahodha wa Japan aliiongoza vyema nchi yake katika michuano ya Asia yam waka 2018. Kumagai amekuwa nahodha tangu mwaka 2018, lakini amekuwa na majukumu hayo tangu kombe la dunia la 2011 dhidi ya Marekani, wakati aliposhinda bao la mkwaju. Ana miaka 28 na tayari ameshinda mataji 100 nchini Japan.

error: Content is protected !!