Ushuhuda wa kijana wa Kichina aliyeupokea Uislamu

Namir Xia, ni kijana wa kichina mwenye umri wa miaka 20 ambaye wiki 7 zilizopita alitoa neno la shahada na kuupokea uislamu, ufuatao ni ushuhuda wake kama alivyolisimulia shirika la la habari la Anadolu (AA).

Xia ni mwanafunzi wa fani mbili tofuti katika chuo kikuu kinachoheshimika nchini Marekani, Chuo kikuu cha New York (NYU), akisomea shahada ya uchumi pamoja na sayansi ya kompyuta. Anasimulia kwamba aliona katika vyombo vya habari taarifa zilizokuwa zikipinga uislamu na ikamfanya atake kujua zaidi kuhusu Quran.

Mwanafunzi huyo anasema tofauti na alichokiona kwenye vyombo vya habari lugha iliyotumika katika Quran ilikuwa kivingine kabisa kitu kilichompa shauku zaidi. Anaendelea kusimulia kwamba baada ya kufikiria na kufanya utafiti kwa mwaka 1 na nusu, wiki 7 zilizopita kabla ya kuanza kwa mwezi wa Ramadhani, alikwenda katika msikiti mmoja uliokuwa karibu akatoa neno la shahada na kuwa muislamu.

Xia anasema kwamba hii ilikuwa ni Ramadhan yake ya kwanza kitu kilichomfanya awe na shauku, pamoja na hilo anasema kwamba amefunga swaumu yake ya Ramadhani.

Xia anaendelea kusimulia kwamba katika mwezi wa Ramadhani alitembelea misikiti mbalimbali iliyokaribu na eneo analoishi, alishangazwa na idadi ya misikiti iliyokuwako eneo hilo kwani hakufahamu kama kulikuwa na misikiti mingi kiasi hicho, alifurahiswa na jinsi waumini walivyokuwa wakiswali swala ya Taraweh.

Xia akielezea  jinsi familia yake ilivyopokea habari ya yeye kuwa muislamu alisema,  familia yake inaishi Baijing, akizungumza nao kwa njia ya simu ya video aliwaambia kwamba ameupokea Uislamu, wakapigwa na butwaa wakabaki wameganda , hawakuongea kwa muda wa dakika moja, mbili. Baadaye wakamuuliza kwa nini lakini. Akawaelezea kwamba Uislamu ni dini ya amani na sio kama baadhi ya watu na vyombo vya habari vinavyotaka uonekane.

error: Content is protected !!