Umoja wa Ulaya wazidi kuisusia Israel, Mogherini akataa kuonana na walowezi wa Kizayuni

Umoja wa Ulaya wazidi kuisusia Israel, Mogherini akataa kuonana na walowezi wa Kizayuni

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amekataa ombi la kundi moja la walowezi wa Kizayuni waliotaka kuonana naye mjini Brussels, Ubalgiji.

Kituo cha upashaji habari cha Palesitna kimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Federica Mogherini amekataa kuoanana na walowezi wa Kizayuni huko Brussels.

Kabla ya hapo pia, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya aliutaka utawala wa Kizayuni uache kujenga vitongoji vya walowezi wake katika ardhi ambazo Israel inawapora Wapalesitna.

Wanajeshi wa Israel wakivunja nyumba za Wapalestina

 

Habari hiyo imethibitishwa pia na redio ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jinai za utawala wa Kizayuni za kuendelea kuwapora Wapalestina ardhi zao na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni zimeikasirisha jamii ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Ulaya.

Asasi za kitaifa na makundi yanayowaunga mkono wananchi wa Palestina yametoa mwito kwa wananchi wa nchi za Ulaya na Marekani wa kususiwa bidhaa zinazozalishwa katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, kwani zimezalishwa katika ardhi walizoporwa Wapalestina.

Umoja wa Mataifa nao umepasisha maazimio mengi ya kusisitiza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalesitna ni kinyume cha sheria.

 

error: Content is protected !!