UJUMBE WA LEO KWA WENYE AKILI

Katika kutoa Zakaah au Sadaka kunaizoesha nafsi katika kuwapendelea kheri watu wenye haja na katika kuwaonea huruma na pia kunaipatia nafsi baraka nyingi kutoka kwa Allaah Subhanahu wa Ta’ala.
Allaah ِAnasema:
وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ
“Na chochote mtakachotoa, basi Yeye Atakilipa; naye ni Mbora wa wanaoruzuku”.
Saba-a – 39

Pia Katika kutoa Zakaah au Sadaka kunaizoesha nafsi katika kuwapendelea kheri watu wenye haja na katika kuwaonea huruma na pia kunaipatia nafsi baraka nyingi kutoka kwa Allaah Subhanahu wa Ta’ala.
Allaah ِAnasema:
وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ
“Na chochote mtakachotoa, basi Yeye Atakilipa; naye ni Mbora wa wanaoruzuku”.
Saba-a – 39

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah anasema: ‘Ewe mwanadamu, toa na sisi tutakupa”

Anasema Ibni Uthaimiyn:
“Kutoa Zakaah ni jambo liliofaradhishwa katika Uislam, na ni nguzo muhimu sana baada ya Shahada mbili na Swalah, na dalili ya kuwajibika kwake imo ndani ya Qurani na pia katika mafundisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), pamoja na ijmai ya Waislam, na yeyote anayeikanusha nguzo hii anakuwa Kafir aliyertadi katika Uislam, na hukumu yake ni kutubishwa, na akitubu anasamehewa. Ama akikataa kutubu na akaendelea kuikanusha basi hukmu yake ni kuuliwa.
Ama anayeifanyia ubakhili au akapunguza katika Zakaah yake, huyo anakuwa miongoni mwa madhalimu wanaostahiki adhabu ya Allaah.
Allaah Anasema:
وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ. يَوْمَ يُحْمَى عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَى بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ هَـذَا مَا كَنَزْتُمْ لأَنفُسِكُمْ فَذُوقُواْ مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ
“Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Allaah, wape habari za adhabu inyoumiza inayowangoja.
Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, (na huku wanaambia); “Haya ndiyo (yale mali) mliyojilimbikia (mliyojikusanyia) nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya) yale mliyokuwa mkikusanya.”
At Tawba – 34 – 35

==============
SWALI JEE UNGEPENDA KUCHANGIA KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA MSKITI UNAOSIMAMIWA NA TAASISI YA SHAIBU FOUNDATION ?

JINSI YA KUCHANGIA:

1. NJIA YA KWANZA:
SASA NI RAHISI ZAIDI, CHANGIA KWA #MPESA, #EZYPESA, #tigopesa n.k:
1. INGIA KATIKA MENU *150*0..#
2. CHAGUA TUMA PESA KWENDA #BENK,
3. CHAGUA BENK YA NMB Bank Plc
4. TUMA KWENDA ACCOUNT NAMBA: 20210010991 (Shaibu Foundation )
5. ENDELEA KWA MUJIBU YA MTANDAO WAKO.

2. NJIA YA PILI:

KWA PITIA BENK:
AKAUNTI NAMBA: 20210010991
JINA LA AKAUNTI: SHAIBU FOUNDATION
BENKI: NMB TANZANIA

Wabi’llah Taufiq,

“EWE MOLA WANGU, SHUHUDIA NIMEFIKISHA UJUMBE WAKO”

JIFUNZE ZAIDI KUHUSU ZAKA

Alhidaaya.com

al-manani

n.k

error: Content is protected !!