TI: Jitihada za Magufuli za kupambana na ufisadi Tanzania zinazaa matunda

Rais John Magufuli

Utendakazi na jitihada za kupambana na ufisadi za Rais John Magufuli wa Tanzania zimeifanya nchi hiyo ya Afrika Mashariki ishike nafasi ya kwanza barani Afrika katika vita dhidi ya ufisadi.

Ripoti mpya ya utafiti uliofanywa na mashirika ya Transparency International (TI) na Afro- Barometer imesema kuwa, Tanzania imeibuka ya kwanza barani Afrika katika kategoria mbili za kupambana na ufisadi na rushwa.

Asilimia 50 ya Watanzania walioshirikishwa kwenye utafiti huo wa Transparency International wanaamini kuwa, licha ya kuweko vizingiti vingi katika vita dhidi ya ufisadi, lakini aghalabu ya wananchi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki wako tayari kuchua hatua za kupambana na ufisadi wa kifedha.

Watu 47,000 wameshirikishwa kwenye utafiti huo uliofanyika kati ya Septemba 2017 and Septemba mwaka jana 2018 katika nchi 35 za bara Afrika. 

Rais Magufuli: Natamani wakati nitakapomaliza muda wangu wa uongozi, Tanzania iwe na mabilionea zaidi ya 100

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa, Tanzania imeipiku Rwanda katika kupambana na ufisadi, kwani mwaka jana Rwanda ilishika nafasi ya kwanza kwa alama 56, ikifuatiwa na Tanzania pointi 36, Uganda (26), Burundi (17) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (19).

Juni mwaka huu, serikali ya Tanzania ilisema kuwa uchumi wa nchi hiyo ulikuwa na kufikia asilimia 7.0 mwaka jana ikilinganishwa na wa asilimia 6.8 mwaka 2017.

error: Content is protected !!