Tembe ya kupanga uzazi ya wanaume imepita majarabio ya awali kwa matumizi ya binaadamu, wataalamu katika mkutano mkuu wa afya wamearifiwa

Mbegu za kiume

Tembe ya kupanga uzazi ya wanaume imepita majarabio ya awali kwa matumizi ya binaadamu, wataalamu katika mkutano mkuu wa afya wamearifiwa.

Tembe hiyo ya kutumiwa mara moja kwa siku ina homoni zilizoundwa kusitisha uwepo wa manii au shahawa.

Inaongezea njia ya ziada ya kupanga uzazi kwa wanaume kando na kutumia mipira ya kondomu na upasuaji wa mirija ya uzazi – mbinu za pekee zinazotumika kwa sasa kwa wanaume.

Lakini madaktari katika kongamano la mwaka la Endocrine Society wamearifiwa kwamba huenda ikachukua muongo mmoja kabla ya dawa hizo ziwasilishwe madukani.

Hamu ya tendo la ndoa

Tembe ya kupanga uzazi kwa wanawake ilizinduliwa Uingereza miaka 50 iliyopita. Basi kwanini tembe ya wanaume inaonekana vigumu kuidhinishwa?

Baadhi wanasema hakujakuwa na azma ya kijamii na kibiashara kushinikiza uzinduzi wake – lakini matokeo ya utafiti wa maoni yanaashiria wanaume wengi wangependa kuitumia iwapo ingepatikana.

Mjadala lakini ni iwapo wanawake watawaamini wanaume kumeza tembe hizo kama inavyostahili.

Ki bayolojia, changamoto ya kuunda tembe ya homoni kwa wanaume ni kuhakikisha haiathiri hamu ya tendo la ndoa au kupunguza uwezo wa mwanamume kushiriki tendo hilo.

Uwepo wa manii

Kwa wanaume walio na uwezo wa kuzalisha, seli mpya za manii zinaundwa katika sehemu nyeti za wanaume kutokana na homoni.

Kuzuia kwa muda hali hii pasi kupunguza viwango vya hamoni kwa kiwango stahili kiasi cha kushuhudiwa madhara.

Lakini tembe hii ya wanaume, inaofanyiwa majaribio na watafiti kutoka taasisis ya LA BioMed na chuo kikuu cha Washington, inatarajiwa kufikia lengo hilo, watafiti wanasema.

Vidonge
Dawa za kupanga uzazi

Majaribio ya awali ya “awamu ya kwanza” yaliofanyiwa kwa wanaume 40 yalikuwa na matokeo mazuri, wataalamu hao waliwaambia wajumbe katika mkutano huo uliofanyika New Orleans.

Katika utafiti huo wa siku 28:

  • 10 walikunywa mfano wa tembe hiyo
  • 30 walikunywa tembe hiyo ya majaribio ya kupanga uzazi kwa wanaume, 11-beta-MNTDC

Na miongoni mwa waliokunywa dawa ya androgen, viwango vya homoni inayohitajika kuunda manii ilipunguwa pakubwa ikilinganishwa na waliokunywa mafno wa tembe hiyo, na vilirudi kwa hali yakawaida baada ya kumalizika majaribio.

Matatizo ya kushiriki tendo la ndoa

Madhara yake kwa upande wmingine yalikuwa machache na madogo.

wanaume watano waliokunywa tembe hiyo waliarifu kupungukiwana hamu ya kushiriki tendo la ndoa , huku wengine wawili wakieleza kukabiliwa na matatizo ya kuweza kushiriki tendo hilo, lakini shughuli yenyewe haikupungua, hakuna mshiriki alyecha kuinywa dawa kutokana na madhara na ilipita viwango vyote vya usalama wa matumizi.

Watafiti walioshughulika, Prof Christina Wang na wenzake, wamefurahia hatua hiyo lakini wana tahadhari kuhusu matokeo yake.

“Matokeo yetu yanayonyesha kwamba tembe hiyo inayojumuisha mifumo miwili ya homoni kwa pamoja itapunguza utengenezaji wa manii huku ikilinda uwezo wa kushiriki tendo la ndoa,” ameeleza.

Lakini majaribio makubwa na ya muda mrefu zaidi yanahitajika kuangalia iwapo zitafanya kazi kama dawa za kupanga uzazi zinavyohitajika.

Kubadilika tabia

wanasayansi wengine wamekuwa wakishughulika kuunda dawa ya upangaji uzazi kwa wanaume kupitia sindano watakayochomwa wanaume kila baada ya miezi miwili.

Lakini waliachana na mpango huo na hawakuendelea na awamu ya pili ya utafiti huo kwa kuangalia usalama na ufanyaji kazi wa sindano hiyo baada ya baadhi ya wanaume waliojitolea kuripoti madhara ikiwemo kubadilika tabia au msongo wa mawazo.

Kwa wanaume ambao hawapendi kumeza dawa za homoni, watafiti wamekuwa wakitafuta njia ya kuzuia mbegu kusafiri na kuzisitisha kutoka kwenye uume – katika mbinu ya kudumu , isiyohusisha upasuaji wa mishipa ya uzazi kwa wanaume.

Mbegu ya kiume
Mbegu ya kiume

Soko la uuzaji dawa

Prof Richard Anderson, wachuo kikuu cha Edinburgh,anaongoza utafiti huo Uingereza utakaofanya majiribio ya matumizi ya mafuta ya kupakwa mwilini mwa mwanamume.

Ameeleza sekta ya famasia imejivuta kukubali mbinu mpya ya kupanga uzazi kwa wanaume ambayo itapokewa vizuri na wanaume wenyewe na hata wanawake.

“Nadhani sekta hiyo haijashiwishika kuhusu wateja katika soko hilo,” amesema.

“Imekuwa hadithi ndefu kwa kweli – sehemu ya tatizo ikiwa ni ukosefu wa uwekezaji.”

error: Content is protected !!