Shirika la ndege la Uturuki (THY) limetoa onyo kwa abiria wake wanaokwenda Tanzania

Shirika la ndege la Uturuki (THY) limetoa onyo kwa abiria wake wanaoenda nchini Tanzania kufuatia serikali ya nchi hio kupiga marufuku matumizi ya mifuko na mikoba ya plastiki.

Taarifa iliyotolewa kupitia tovuti rasmi ya THY inasema kwa mujibu maamuzi yaliyofanywa na serikali ya Tanzania kuanzia Juni 1, mifuko yote na mikoba ya plastiki haitaruhusiwa kuingia nchini humo.

Taarifa hiyo imeendelea kusomeka kwamba shirika hilo linawashauri abiria wake wanaoelekea nchini humo kutokubeba mfuko au mkoba wowote wa plastiki katika mizigo yao.

error: Content is protected !!