Shirika la kutengeneza magari la Fiat chrysler limeondoa pendekezo lake la kuungana na shirika la Renault

Fiat Chrysler shirika la utengenezaji magari lenye makao yake makuu nchini Italia limeondoa mpango wake wa kuungana na shirika la utengenezaji magari la Ufaransa Renault Group.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Fiat Chrysler ni kwamba baada ya kuutathmini kwa umakini mpango huo wa kuungana, kwa manufaa ya mashirika hayo yote mawili wameamua wausitishe mpango huo. Sababu kubwa ni kutokana na hali ya kisiasa ilivyo nchini Ufaransa.

Mei, 27 mwaka uliopita  shirika Fiat Chrysler Automobiles, (FCA),  lilitoa pendekezo la kuungana  kwa hisa za asilimia hamsini kwa hamsini na shirika la Renault.

Shirika la Renault lilianzishwa mwaka 1898, mwaka uliopita liliuza magari milioni 3,9 katika nchi 134, shirika hilo lina taasisi za kuzalisha magari zipatazo 36 , lina  wafanyakazi zaidi ya laki 1 na elfu 80  na vituo vya mauzo vipatavyo 12 elfu na 700. Ufaransa inamiliki asilimia 15 ya shirika hilo.

error: Content is protected !!