Ripoti ya WHO kuhusu hali ya kiakili ya waathirika wa vita

Matokeo ya utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonyesha kuwa moja ya tano ya watu wanaoishi katika maeneo yaliyoathiriwa na vita wanaugua maradhi ya kiakili.

Shirika la Afya Duniani limeripoti kuwa mtu mmoja kati ya watano wanaoishi katika maeneo yaliyoathiriwa na vita wamepatwa na matatizo ya msongo wa mawazo na kukumbwa na hali ya wasiwasi baada ya kuathirika kisaikolojia huku wengine wengi wakipatwa na maradhi makubwa ya kiakili. Shirika la WHO limeongeza kuwa matokeo ya uchunguzi wao yanaashiria kuwepo taathira za muda mrefu za migogoro inayosababishwa na vita katika nchi mbalimbali zikiwemo Afghanistan, Iraq, Sudan Kusini, Syria na Yemen. Takwimu za Umoja wa Mataifa pia zinaonyesha kuwa mwaka 2016 mapigano yaliongezeka sana na kwamba asilimia 12 ya watu duniani wanaishi katika maeneo yanakojiri vita. 

Matokeo  hayo yanatokana na utafiti wa Afya ya Akili uliofanywa na Shirika la Afya Duniani kuhusu chunguzi 129 zilizochapishwa na nchi 39 kati ya mwaka 1980 na 2017. Aidha maeneo ambayo miaka kumi iliyopita yalikumbwa na mapigano yamechunguzwa kupitia utafiti huo; huku magonjwa ya kiakili yakikadiriwa kuwa ya kiwango cha wastani au cha juu zaidi. Majanga ya kimaumbile au milipuko ya magonjwa kama Ebola pia hayajaorodheshwa katika utafiti huo wa WHO. Nchi zilizotajwa na WHO ni zile zilizoathiriwa na uingiliaji wa kijeshi wa Ulaya na Marekani. 

error: Content is protected !!