Rais Ruhani asema Iran itaridhia kama Marekani itatubu na kuomba radhi

Rais wa Iran Hasan Ruhani amesema kwamba kama Marekani itatubu na kuiomba radhi Iran kwa mabaya yote iliyoyafanya  kipindi cha nyuma dhidi yake, Basi Iran itaridhia toba hio.

Ruhani aliyasema hayo mjini Tehran ambapo alikuwa akijadili sera za Marekani dhidi ya Iran katika mkutano na mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali.

Ruhani alisema umefika muda sasa majeshi yote ya kigeni yaondoke katika kanda na yaache kuingilia mambo ya nchi zingine, aliongeza kwamba Marekani kamwe haitofikia malengo yake.

Ruhani alisema ni kwa miaka 40 sasa ambapo Marekani imetumia kila aina ya mbinu ili iweze kuitawala Iran lakini hawajafanikiwa.

Kuhusu mustakabali wa uhusiano wa Iran na Marekani Ruhani alisema kwamba sera za Iran ni kuwa na mahusiano mazuri na dunia nzima, kama Marekani ikitubu na kuomba radhi kwa vitimbi vyote ilivyoifanyia Iran, Iran itakuwa tayari kuikubali toba ya Marekani.

error: Content is protected !!