Quiin Abenakyo kutoka Uganda awa mrembo wa dunia namba tatu

Mrembo Vanessa Ponce De Leon kutoka Mexico ametawazwa kuwa mrembo wa dunia “miss world” kwa mwaka 2018. Mashindano hayo ya kumtafuta mrembo wa dunia yalifanyika Jumamosi usiku mjini Sanya katika Jimbo la Hainan nchini China.

Mrembo kutoka Thailand Nicolene Pichapa Limsnukan alishika nafasi ya pili katika mashindano hayo. Mrembo kutoka nchini Uganda Quiin Abenakyo alishika nafasi ya tatu.

Baada ya sherehe ya kutoa zawadi kukamilika warembo 118 kutoka mataifa mbalimbali walivaa nguo za asili za mataifa yao na kupeperusha bendera za nchi zao.

Hii ni mara ya nane kwa kwa mji wa Sanya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo. 

error: Content is protected !!