Wahamiaji haramu 13 wakamatwa katika operesheni ilioendeshwa mkoani Edirne

Wahamiaji haramu 13 wakamatwa katika operesheni ilioendeshwa mkoani Edirne

Kimataifa
Wahamiaji haramu 13 wamekamatwa katika operesheni ilioendeshwa  mkoani Edirne. Edirne ni mkoa  unaopatika Kaskazini-Magharibi mwa Uturuki. Wahamiaji haramu hutumia eneo  hilo kuingia kinyume cha sheria nchini Ugiriki na Bulgaria. Kikosi cha kulinda mipaka kimewakamata wahamiai hao waliokuwa katika gari  katika kijiji ch Adasarhanlı mkoani Edirne. Wahamiaji hao raia kutoka nchini Irak akiwemo pia raia mmoja kutoka Pakistani.
Mpango wa kundi la amani la Libya wa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo

Mpango wa kundi la amani la Libya wa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo

Kimataifa
Mkuu wa kundi la amani la Libya amesema kuwa kumependekezwa mpango mpya wa kitaifa kwa ajili ya kurejesha amani nchini humo. Youssef Kashoune ambaye pia ni mjumbe wa kundi la makamanda wa zamani wa nchi hiyo amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Tunisia akiwa pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kiraia ya Libya kuwa mpango uliopendekezwa kwa shabaha ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo umezingatia mirengo yote ndani ya Libya. Kashoune ameongeza kuwa mpango huo umezingatia matakwa ya wananchi wa Libya katika kuwashughulikia raia maskini, wakimbizi na kutatua migogoro inayotokana na kuenea ufisadi na ugaidi nchini humo. Amesema mpango huo unajumuisha pia suala la kuhitimisha mapigano na kuyavunja makundi yenye silaha kama hatua ya mwanzo ya kurejesha aman
Mama mzazi ndio sababu ya Kylian Mbappe kukosa dili hili

Mama mzazi ndio sababu ya Kylian Mbappe kukosa dili hili

Michezo
Aliyekuwa ‘scout’ wa klabu ya Chelsea, Daniel Boga amesema kuwa mama mzazi wa nyota wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ndiye aliyesababisha kinda huyo kuondoka Stamford Bridge mwaka 2012. Mfaransa huyo, Mbappe amewahi kufanya majaribio ‘the Blues’ akiwa na umri wa miaka 13 na kuitumikia timu ya vijana ili kuendelea kuonyesha uwezo zaidi. Lakini kwa mujibu wa Boga, klabu hiyo ya ligi kuu England haikuvutiwa na kiwango alichokionyesha na hivyo kumuomba kurudi kwa awamu nyingine kwaajili ya majaribio lakini, Fayza Lamari ambaye ni mama mzazi wa mchezaji huyo akakataa. ”Nilimleta yeye na familia yake, alikuwa mwenye ujuzi kama aliyo nao hivi sasa na alicheza dhidi ya Charlton na kushinda mabao 7 – 0,” amesema Boga. Boga ameongeza ”Katika ile wiki yake akiwa Chelsea, tulikwenda ofi
Maziko ya Kofi Annan yahudhuriwa na viongozi wa kimataifa Ghana

Maziko ya Kofi Annan yahudhuriwa na viongozi wa kimataifa Ghana

Kimataifa
Wanajeshi wanaobeba jeneza kwa kulipa heshima stahiki wakiwa pembeni ya jeneza la Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan aliyeaga dunia huko Uswitz, kabla ya maziko ya kitaifa, ukiwa eneo la Uwanja wa ndege wa Jubilee Accra, Ghana. Raia wa Ghana wameendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN) Kofi Annan, wakati maandalizi ya kumzika Alhamisi yakiwa yamekwisha kamilika. Mwili wake Annan umewekwa kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Accra ambapo ibada ya kumuaga inafanyika kabla ya kuzikwa Alhamisi. Wageni waheshimiwa kutoka kote duniani wanahudhuria mazishi ya kiongozi huyo. Kati yao akiwemo Katibu Mkuu wa UN wa sasa Antonio Gutterrez na Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast. Vyombo vya habari nchini G...
Shirika la Posta Tanzania (TPC) Lajizatiti Kimataifa Katika Huduma Zake.

Shirika la Posta Tanzania (TPC) Lajizatiti Kimataifa Katika Huduma Zake.

Biashara & Uchumi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati akiwakaribisha waandishi wa habari katika mkutano ambao Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (hayupo pichani), alielezea masuala mbalimbali ya shirika katika kujiimarisha kimataifa, ambayo waliyatoa katika mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Mashirika ya Posta duniani (UPU), uliofanyika Adis Ababa, Ethiopia, hivi karibuni. Kulia ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe na kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika Macrice Mbodo. Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC),  Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (kulia), akielezea masuala mbalimbali ya shirika hilo, katika kujiimarisha kimataifa, ambayo waliyatoa katika mkutan
error: Content is protected !!