Marekani: Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vitaendelea kuwepo

Marekani: Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vitaendelea kuwepo

Biashara & Uchumi
Serikali ya Marekani haitaondoa vikwazo ilivyoiwekea Zimbabwe hadi pale serikali mpya ya Rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo itakapodhihirisha kuwa inabadili mielekeo yake. Hayo yameelezwa na afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya uchumi wa Marekani. Naibu Waziri wa Uchumi na Masuala ya Biashara wa Marekani, Manisha Singh amesema kuwa watu na taasisi 141 za Zimbabwe akiwemo Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe wako chini ya vikwazo vya Marekani.  Amesema mashinikizo ya Marekani kwa Zimbabwe bado yako palepale. Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe Amedai kuwa Washington inajaribu kutumia njia ya mashinikizo ili kushawishi mageuzi ya kisiasa na kiuchumi na kuheshimiwa haki za binadamu. Naibu Waziri wa Uchumi na Masuala ya Biashara wa Marekani ameon
Waislamu katika zaidi ya nchi 41 duniani wamkumbuka Ali Asghar, shahidi wa miezi 6 wa Karbala

Waislamu katika zaidi ya nchi 41 duniani wamkumbuka Ali Asghar, shahidi wa miezi 6 wa Karbala

Jamii
Shughuli ya kimataifa ya kukumbuka mtoto mchanga wa Imam Hussein bin Ali (as) aliyeuwa shahidi katika medani ya Karbala imefanyika leo nchini Iran na katika nchi nyingine zaidi ya 40 ikiwashirikisha wapenzi na wafuasi wa Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw). Mjini Tehran, shughuli hiyo ya kidini ilianza mapema leo katika msikiti mkubwa wa Imam Khomeini ikiwashirikisha kinamama waliokuwa wamebeba watoto wachanga wanaonyonya. Shughuli hiyo imeandamana na qasida, mashairi na tungo zinazowakumbuka mashahidi wa Karbala hususan Ali al Asghar, shahidi mchanga zaidi kati ya mashahidi waliouliwa wakiwa pamoja na mjukuu wa Mtume (saw), Imam Hussein (as) katika siku ya Ashuraa. Wairan wamkumbuka Ali al Asghar (as).  Shughuli kama hiyo imefanyika pia katika nchi 41 duniani ambako kinamama waliokuw
Sheria ya kura ya maoni kuhusu katiba ya Libya yapasishwa

Sheria ya kura ya maoni kuhusu katiba ya Libya yapasishwa

Siasa
Bunge la Libya lenye makao yake mashariki mwa nchi limefanya kikao cha dharura na kupasisha suala la kufanyika kura ya maoni kuhusu katiba ya nchi hiyo. Abdullah Bliheeq msemaji wa Bunge la Libya lenye makao yake katika mji wa Tobruk amesema kuwa licha ya kupasishwa sheria hiyo Bunge hilo pia limechukua uamuzi wa kufanya kikao cha kuchunguza marekebisho, lengo likiwa ni kuzuia kubadilishwa sheria hiyo. Spika wa bunge hilo la Libya, Aguila Saleh amewataka wabunge kuitisha kikao kujadili sheria hiyo ya kura ya maoni. Libya imetumbukia katika hali ya machafuko, hujuma za makundi yenye silaha na kuwa ngome ya makundi ya kigaidi kutokana na matukio yaliyojiri nchini humo mwaka 2011 na uingiliaji wa Marekani na muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi (Nato) nchini humo. Ushindani wa
Romelu Lukaku: Mkufunzi wa Man Utd Jose Mourinho ‘hawezi kuficha hisia zake’

Romelu Lukaku: Mkufunzi wa Man Utd Jose Mourinho ‘hawezi kuficha hisia zake’

Michezo
Romelu Lukaku alijiunga na United kutoka Everton kwa dau la £75m mwaka 2017 Jose Mourinho hadanganyi na hawezi kuficha hisia zake kama wakufunzi wenzake katika ligi ya Uingereza , kulingana na mshambulijia wa United Romelu Lukaku. Mkufunzi wa United Mourinho alitaka kupewa heshima na vyombo vya habari baada ya kukasirika katika mkutano na wanahabari baada ya timu yake kupoteza 3-0 nyumbani dhidi ya Tottenham mwezi Agosti. Lakini Lukaku anasema kuwa raia huyo wa Ureno ni mtu wa familia , ''huwafanya wachezaji kucheka na anawapigania'' , hivyobasi anahitaji heshima. ''Watu wanajua kwamba ana upande unaomfanya kuwa mshindi'', alisema Lukaku. 'Lakini kile ninachompendea hawezi kuficha hisia zake. Wakati anapokasirika utajua amekasirika, anapofurahi utajua anafurahi''. ''Sijui kw
TANESCO Yawasha Kituo Kipya Cha Kupoza na Kusambaza Umeme Madaba Mkoani Ruvuma.

TANESCO Yawasha Kituo Kipya Cha Kupoza na Kusambaza Umeme Madaba Mkoani Ruvuma.

Biashara & Uchumi, Mikoani
Kituo kipya na cha kisasa cha Madaba Mkoani Ruvuma kikiwa kimewashwa rasmi usiku wa kuamkia Septemba 13, 2018. Ujenzi wa kituo hicho ambao ulianza mwaka 2017, ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea wa msongo wa 220/33kV na sasa Songea imeunganishwa na Gridi ya Taifa na tayari mitambo ya kufua umeme wa jenereta iliyoko Songea mjini imezimwa rasmi, amethibitisha  Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO Bi. Leila Muhaji. HISTORIA imeandikwa upya kwa wakazi wa mji wa Songea na viunga vyake, baada ya serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwasha kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 220/33kv cha madaba usiku wa kuamkia Septemba 13, 2018. Kituo hicho ni sehemu ya vituo vipya vitano vilivyojengwa chini ya mradi wa umeme Makambaka- Songea. K
error: Content is protected !!