Dk. Sira: Wakandarasi tangulizeni uzalendo

Dk. Sira: Wakandarasi tangulizeni uzalendo

Nyumbani
WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, imewataka watendaji wa ujenzi wa barabara kuwa wazalendo na nchi yao kwa kutengeneza barabara zanye kiwango na zitakazoweza kudumu kwa muda mrefu. Waziri wa wizara hiyo, Dk. Sira Ubwa Mamboya, alieleza hayo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea barabara ya njia kongwe Chake – Wete, ambayo ipo katika matayarisho ya kujengwa upya. Alieleza ipo haja ya kuwatumia wakandarasi wa ndani baada ya kutegemea kutoka nje ya nchi, kwani kwa sasa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari imeamua kununua vifaa vya ujenzi ambavyo vitasaidia kujenga barabara. Waziri huyo alisema, serikali imekuwa ikitumia pesa nyingi kwa wakandarasi kutoka nje ya nchi kwa kujenga barabara na hatimae wanapitisha muda wa makubaliano, huku barabara nyengine zikijengwa chini y
Watafiti wamepata mabaki ya pombe ya zamani zaidi duniani mjini Haifa, Israel

Watafiti wamepata mabaki ya pombe ya zamani zaidi duniani mjini Haifa, Israel

Biashara & Uchumi
Wataalamu wa vitu vya jadi wakitafuta ushahidi wa vyakula vya mimea baada ya kugundua mabaki ya pombe Watafiti wamefichua kiwanda cha pombe kilicho na mabaki ya pombe yaliodumu takriban miaka 13,000 iliopita katika pango la zamani karibu na mji wa Haifa nchini Israel. Walifikia ugunduzi huo wakati walipokuwa wanafanya uchunguzi kuhusu eneo la makaburi ya jamii ya wafugaji wa kuhama hama ambao walikuwa wawindaji. Utengenezaji wa pombe unadhaniwa kuwepo tangu miaka 5,000 iliopita lakini ugunduzi huu huenda ukabadili historia ya utengenezaji wa kinywaji hicho. Ugunduzi huo pia huenda usiashirie kuwa kileo hicho kilitumika kuoka mikate kama ilivyodhaniwa. Wanasayansi wanasema hawana uhakika ni kitu gani kilivumbuliwa kwanza kati ya pombe na mkate. Vitalu vya vifuniko vilipatikana ...
Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar Wamtembelea Mwenyekiti wa ZFA Mstaaf Ali Ferej Tamim Nyumbani Kwake Shangani Zanzibar.

Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar Wamtembelea Mwenyekiti wa ZFA Mstaaf Ali Ferej Tamim Nyumbani Kwake Shangani Zanzibar.

Michezo
Katibu wa kamati ya mpito inayosimamia  masuala ya soka visiwani Zanzibar kwa sasa Khamis Abdallah Said akizungumza na aliyekuwa rais wa chama cha mpira wa miguu visiwanibZanzibar Ali Fereji wakati alipotembelea nyumbani kwake pamoja na waandishi mbali mbali wa michezo . Mwenyekiti wa Zamani wa Chama Cha Mpira Zanzibar ZFA Ali Ferej Tamim akizungumza na mwandishi wa habari za Michezo Zanzibar Ndg. Salu Vuai walipofika nyumbani kwake shangani kumtembelea na kumjulia hali yake. Waandishi wa habari za michezo Zanzibar wakimtembelea na kumjulia hali Mwenyekiti Mstaaf wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar ZFA Ali Ferej Tamim walipofika nyumbani kwake shangani Zanzibar.  
Askofu Mkuu wa New York: Kashfa za ngono zinavunja imani ya watu kwa kanisa Katoliki

Askofu Mkuu wa New York: Kashfa za ngono zinavunja imani ya watu kwa kanisa Katoliki

Kimataifa
Askofu Mkuu wa New York nchini Marekani amezungumzia kashfa kubwa ya vitendo vya kuwanajisi watoto katika kanisa Katoliki na kusema kuwa, hali hiyo itaondoa imani ya watu kwa taasisi hiyo ya kidini. Timothy M. Dolan amesema kuwa maafa ya kuwanajisi watoto yanayofanywa na makasisi na wachungaji wa kanisa Katoliki ni mithili ya kuvuja kwa mavuta ya petroli na kuchafua bahari na kwamba kwanza huwasibu wahanga na familia zao. Askofu Mkuu wa New York ameongeza kuwa, sehemu kubwa ya maafa ya kashfa za ngono za makasisi na wachungaji huonekana pale waumini wa kanisa hilo wanapowaambia maaskofu kwamba, "ni vigumu sana kuwaamini nyinyi". Ameongeza kuwa hii ni licha ya kwamba, kanisa limejengwa kwa msingi wa imani ya watu na si kwa mabavu na ubabe. Afisa huyo wa ngazi za juu wa kanisa Katoli...
Kiongozi wa upinzani Zimbabwe aakhirisha kula kiapo

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe aakhirisha kula kiapo

Siasa
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe ameakhirisha mipango ya kushiriki katika hafla ya kujiapisha kama rais wa nchi iliyokuwa imepangwa kufanyika leo (Jumamosi) baada ya polisi kupiga marufuku mikutano na mijumuiko ya wananchi kufuatia nchi hiyo kuathiriwa na mlipuko wa kipindupindu kilichouwa watu 26 hadi sasa. Nelson Chamisa kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC amesema kuwa kulifanyika udanganyifu katika matokeo ya uchaguzi wa Julai 30 yaliyompa ushindi Rais Emmerson Mnangagwa. Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza kufanyika Zimbabwe tangu Robert Mugabe aenguliwe madarakani katika kile kinachotajwa kuwa ni mapinduzi ya jeshi ya mwezi Novemba mwaka jana. Wakosoaji wa Chamisa wanamtuhumu kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe kwamba, anajaribu kumuiga kioongozi wa upinz...
error: Content is protected !!