Yemen na Umoja wa Mataifa zakubaliana kuanzisha korido ya kitiba ya anga

Yemen na Umoja wa Mataifa zakubaliana kuanzisha korido ya kitiba ya anga

Kimataifa
Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen jana zilisaini makubaliano ya kuanzisha korido ya kitiba ya anga kwa lengo la kuwasafirisha nje ya nchi majeruhi wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, wagonjwa na majeruhi wa vita huko Yemen wanaweza kupatiwa matibabu nje ya nchi kwa muda wa miezi sita. Makubaliano hayo yanatazamiwa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 18 mwezi huu. Duru za Yemen zimearifu kuwa kwa mujibu wa makubaliano hayo yaliyosainiwa kati ya Yemen na Umoja wa Mataifa, Saudi Arabia haina haki kuzuia ndege zilizowabeaba majeruhi wa vita na wagonjwa wengine wa Yemen. Ndege za kivita za muungano vamizi huko yemen unaoongozwa na Saudi Arabia hadi sasa umeushambulia mara kadhaa uwanja wa ndege wa Sana'a ili kuzuia kuruka ndege yoyote katika uwanja huo wa kimat
Faith Fennidy: Nywele za binti huyo zenye asili ya kiafrika zimezua mjadala katika mitandao ya kijamii Louisiana, Marekani

Faith Fennidy: Nywele za binti huyo zenye asili ya kiafrika zimezua mjadala katika mitandao ya kijamii Louisiana, Marekani

Jamii
Faith Fennidy, akifuta machozi baada ya kushambuliwa kwa maneno kuhusu nywele zake Video moja iliyotandaa mitandaoni inamuonesha msichana akiondoka shuleni kwasababu ya kuvunja sheria za shule imezua mjadala katika mitandao ya kijamii juu ya ubaguzi na ukosefu wa ufahamu kuhusu nywele za watu weusi. Msichana huyo ana umri wa miaka kumi na mmoja anaitwa Faith Fennidy, anaonekana kwenye video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao pendwa wa facebook, anaonekana akifuta machozi huku akikusanya vitu vyake katika shule ya Christ the King Parish iliyoko Terrytown, Louisiana. Mama wa binti huyo Montrelle amemtaka mwalimu aeleze kwanini rasta za mwanawe zilizofungwa nyuma ya kisogo chake, ni kwa namna gani zimekiuka sera za shule. Shule hiyo ya binafsi imetoa msimamo wake kwa kueleza kuwa wasicha...
Serikali ya Pakistan yalaumiwa kwa kushindwa kulinda usalama wa Waislamu wa madhehebu ya Shia

Serikali ya Pakistan yalaumiwa kwa kushindwa kulinda usalama wa Waislamu wa madhehebu ya Shia

Kimataifa
Jaji Mkuu wa Pakistan amesema kuwa serikali zote zilizotawala nchi hiyo zimeshindwa kulinda usalama na maisha ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na kuzuia mauaji yao mbele ya mashambulizi ya kigaidi yanayolenga wafuasi wa madhehebu hiyo. Saqib Nisar amesisitiza kuwa serikali zote zilizoshika madaraka nchini humo hazikuchukua hatua za maana za kusitisha mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na kusimamisha jinai na mashambulizi ya kigaidi yanayowalenga. Matamshi haya yaliyotolewa na kiongozi wa juu kabisa wa mahakama za Pakistan yamepewa mazingatio makubwa hususan katika kipindi hiki cha mwanzoni mwa mwezi wa Muharram ambapo kuna uwezekano mkubwa wa makundi ya kigaidi na kiwahabi kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya maeneo ya ibada na misikiti ya Waislamu hao. Watu wa Pakistan, M
Kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa Rwanda na shinikizo la jumuiya ya kimataifa

Kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa Rwanda na shinikizo la jumuiya ya kimataifa

Siasa
Wachambuzi wa siasa za Rwanda wanasema kwamba hatua ya Baraza la Mawaziri kuwaachia huru wafungwa Jumamosi inafuatia tetesi kuwa jumuiya za kimataifa imeitaka Rwanda kuwaachilia huru wapinzani wa Rais Paul Kagame. Vyanzo vya habari vinaripoti kuwa hii inatokana na serikali ya Rwanda kuwa imedhamiria kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa nchi za madola mwaka 2020. Pamoja na kuachiliwa wafungwa 2140 Jumamosi wanasiasa wa upinzani wanaendelea kushinikiza kuachiliwa kwa mwanasiasa Diana Rwigara kuachiliwa huru. Kati ya hao waliopewa msamaha Jumamosi ni Kizito Mihigo na Victoire Ingabire Umuhoza, na wengine kati ya hao hukumu zao zilibadilishwa kwa uwezo aliopewa Rais kufuatia maombi yao ya hivi karibuni juu ya kupewa msamaha Juni 2018. Diana, ambaye alikuwa mpinzani...
Wanasheria wa Algeria: Ufaransa inapasa kuwalipa fidia wahanga wa ukoloni nchini Algeria

Wanasheria wa Algeria: Ufaransa inapasa kuwalipa fidia wahanga wa ukoloni nchini Algeria

Jamii
Mwanasheria mmoja wa haki za binadamu nchini Algeria ametaka Paris ilipe gharama na fidia kufuatia kukiri serikali ya Ufaransa kuwatesa na kuwaua wale wote waliokuwa wakiunga mkono mapinduzi ya Algeria. Muhammad Sami Abdulhamid mwanasheria wa nchini Algeria amesema kuwa Paris inapasa kuzilipa fidia familia za wahanga wa kipindi cha kukoloniwa Algeria na hiyo ni kufuatia Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kukiri na kumuomba radhi mke wa mmoja wa wafuasi wa mapinduzi ya Algeria ambaye aliaga dunia baada ya kuteswa na Wafaransa. Maurice Audin alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kifaransa ambaye alikuwa akiishi Algiers mji mkuu wa Algeria miaka kadhaa kabla ya kupata uhuru nchi hiyo; na alikuwa akiunga mkono mapinduzi dhidi ya wakoloni wa Kifaransa. Wanajeshi wa Ufaransa walimtia mbaroni
error: Content is protected !!