Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Manispa ya Guilin China.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Manispa ya Guilin China.

Nyumbani
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif akimpongeza Mkulima maarufu wa mazao ya Chenza maarufu kwa jina la Konco Bibi Lai Yumei alipomtembea  shambani kwake kuangalia taaluma anayotumia katika kilimo hicho.  Picha na – OMPR – ZNZ. Na.Othman Khamis OMPR. Serikali ya Manispaa ya Guilin katika Jimbo la Guangxi Nchini China iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha kwa pamoja masuala yaliyomo ndani ya  Sekta za Utalii, Kilimo na Mazingira kwa nia ya kustawisha Uchumi wa Wananchi wa pande hizo mbili. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Meya wa Manispaa ya Guilin Bibi Wei Fengyun kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Shangrila Spa wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake walipofanya ziara ya Siku mbili kwenye Manispaa hiyo kuangalia miradi ya m
Msanii Bongo Fleva akutwa ugangani live bila ya chenga

Msanii Bongo Fleva akutwa ugangani live bila ya chenga

Michezo
Mkali wa muziki wa singeli Dullah Makabila ameonekana akiwa katika mazingira ya ugangani huku picha na videos zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akifanyiwa vitendo vinavyoashiria kuwa ni vya kishirikina. Miezi kadhaa nyuma mkali huyo wa wa singeli aliwahi kuzungumza na kusema kuwa anaamini imani za kishirikina katika kazi za muziki wake ili kufanikiwa na aliongezea kwa kusema kuwa asilimia kubwa ya wasanii nchini wanatumia ushirikina ili wafanikiwe katika muziki. Kutokana na picha hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii mashabiki wamezidi kubaki na viulizo huku wengi wakiamini kuwa huenda akawa anafanya kiki kwaajili ya video ya ngoma yake mpya na wengine wakihisi kuwa ni kweli.     CHANZO: ZANZIBAR 24
Qassemi amempongeza Mohamed al Halbusi, kuchaguliwa Spika wa bunge la Iraq

Qassemi amempongeza Mohamed al Halbusi, kuchaguliwa Spika wa bunge la Iraq

Siasa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepongeza kuchaguliwa Spika wa bunge la Iraq na wabunge waliochaguliwa na wananchi. Mohamed Al Halbusi amechaguliwa kuwa Spika wa duru ya nne ya bunge la Iraq kwa kura nyingi za wabunge. Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepongeza uchaguzi huo na kuwahutubu Mohamed Al Halbusi Spika Mpya wa bunge la Iraq, wabunge wengine na wananchi kwa kusema kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote inaunga mkono demokrasia, umoja wa ardhi ya nchi hiyo na mamlaka ya kitaifa ya Iraq na inaunga mkono maamuzi ya wabunge wanaochaguliwa na wananchi. Mohamed al Halbusi, Spika mpya wa bunge la Iraq  Qassemi amesema kuchaguliwa Spika wa bunge la Iraq ni hatua muhimu na ya dharura kwa ajili ya kuunda serikali mpya huko Iraq na akasema anat
Ukosefu wa fedha watajwa kufanya vibaya timu za Pemba

Ukosefu wa fedha watajwa kufanya vibaya timu za Pemba

Michezo
BAADHI ya klabu zilizoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora kutoka Pemba na wadau wa wamesema, moja ya sababu kubwa iliyopelekea timu hizo kufanya vibaya msimu huu ni kutokana na ukosefu wa fedha unaoukabili klabu hizo. Zimesema hivi sasa ligi imekuwa na gharama kubwa, kuanzia maandalizi ya usajili na kuwaweka kambini wachezaji. Waliitaja sababu nyengine ni ukosefu wa udhamini katika ligi hiyo ambao pia ulichangia kwa kiasi kikubwa kwa timu za Pemba kufanya vibaya katika ligi hiyo. Mmoja wa viongozi wa Opec ya Pandani, Ali Omar ‘MECCO’, alisema, timu yao ilishindwa kuhimili mikimikiki ya ligi hiyo, kwa kutokuwa na fedha za kuwaweka wachezaji pamoja kambini. Ukitizama tokea unaanza usajili, fedha nyingi zinahitajika, hujacheza unahitaji fedha, sisi tulikuwa tunatok
Marekani yataka Zimbabwe itekeleze ahadi ndipo vikwazo viondolewe

Marekani yataka Zimbabwe itekeleze ahadi ndipo vikwazo viondolewe

Siasa
Balozi Brian Nichols Balozi mpya wa Marekani nchini Zimbabwe, Brian Nichols, amesema kuwa Zimbabwe lazima itekeleze ahadi ya mageuzi iliyotangaza iwapo inataka vikwazo ilivyowekewa na Marekani viondolewe. Katika mahojiano Ijumaa na VOA katika jengo la makao makuu ya Sauti ya Amerika, Washington, DC, Balozi Nichols amesema kuwa serikali mpya iliochaguliwa Zimbabwe ya Rais Emmerson Mnangagwa itapata kuungwa mkono kikamilifu na serikali ya Marekani ikiwa itatekeleza mabadiliko ya kisheria iliyo ahidi wakati wa kampeni za uchaguzi. Amesema mageuzi hayo ni pamoja na kufuata utawala wa sheria na kuruhusu wananchi uhuru wao wa kupasha habari na uhuru wakueleza wanachotaka. Vikwazo vyarudishwa upya Mwezi uliopita, Rais wa Marekani Donald Trump alirudisha vikwazo upya dhi...
error: Content is protected !!