Tesla kupunguza maelfu ya wafanyakazi

Tesla kupunguza maelfu ya wafanyakazi

Biashara & Uchumi
Shirika la kutengeneza magari ya kutumia umeme la nchini Marekani Tesla, kupunguza wafanyakazi wapatao elfu 3. Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, ınasema mkurugenzi mkuu na mwanzilishi wa shirika hilo Elon Musk, aliwatumia ujumbe wa kielectronık wafanyakazi wa shirika hilo na kuwafahamisha kwamba magari yao wanayoyatengeneza bado ni ya gharama kubwa kwa watu walio wengi. Musk alisema inabidi waje na teknolojia mpya ya kisasa itayokuwa ya beı nafuu kuwawezesha kupunguza gharama za uzalıshajı, Ila kwa sasa imewalazimu kupunguza asilimia 7 ya wafanyakazi.
Muungano wa wafanyakazi Tunisia waitisha mgomo wa nchi nzima

Muungano wa wafanyakazi Tunisia waitisha mgomo wa nchi nzima

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa
Muungano wenye nguvu wa wafanyakazi nchini Tunisia UGTT jana (Jumamosi) ulitoa mwito wa kufanyika mgomo wa nchi nzima wa siku mbili mwezi ujao wa Februari ili kushinikiza kupandishwa mishahara ya wafanyakazi laki sita na sabiini elfu (670,000) wa sekta ya umma. Huduma za reli, mabasi, anga na nyinginezo zote zilisimama nchini Tunisia siku ya Alkhamisi huku mitaa ikijaa waandamanaji katika mgomo wa nchi nzima ulioitishwa kuishinikiza serikali iliyokataa kuwapandishia mishahara wafanyakazi wa umma. Mkuu wa muungano huo wa vyama vya wafanyakazi, Nourredine Taboubi amewaambia waandishi wa habari kuwa, "baada ya kushindwa mazungumzo na serikali..., UGTT imeamua kuitisha mgomo mwingine wa nchi nzima tarehe 20 na 21 mwezi ujao wa Februari." Kwa mujibu wa shir...
Wilaya ya Kusini Unguja Tatizo la Utoro na Udhalilishaji Umepungua Shehia ya Mzuri

Wilaya ya Kusini Unguja Tatizo la Utoro na Udhalilishaji Umepungua Shehia ya Mzuri

Jamii, Nyumbani
Imeelezwa kwamba tatizo la utoro, udhalilishaji  wanafunzi kijinsia, uchakavu wa jengo la skuli pamoja na ukosefu wa maji safi na salama katika Shehia ya Mzuri wilaya ya Kusini Unguja ni miongoni mwa matatizo ambayo yameshapatiwa ufumbuzi kufuatia wana kijiji hao kupaza sauti zao na kuwataka viongozi wa Halmashauri kuwatatulia matatizo yao yanayowakabili. Wakizungumza na Zanzibar Leo kwa nyakati tofauti wakazi wa Shehia ya Mzuri wamesema kuja kwa Mradi wa Kukuza Uwajibikaji (PAZA) kumewasaidia kwa kiasi kikubwa kuelezea matatizo yao na kufanyiwa kazi na Serikali. Akiongea kwa niaba ya wananchi wenzake Bi Zawadi Hamdu Vuai (53) mkaazi wa shehia ya Mzuri amesema utoro na vitendo vya udhalilishaji kwa wanafunzi ambao ulikuwa ukifanyika katika shehia yao hivi sasa umepata af
Mapokezi ya Meli ya Sea Star ilipowasili Bandari ya Wete

Mapokezi ya Meli ya Sea Star ilipowasili Bandari ya Wete

Biashara & Uchumi, Nyumbani
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman alizungumza na viongozi na wananchi waliofika katika bandari ya Wete kwa ajili ya kupokea meli ya Sea Star inayomilikiwa na kampuni ya Sea Feries. MELI ya Sea Star ikiwa karibu na gati ya Wete,ikitokea katika bandari ya Unguja MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman akiwa pamoja na viongozi na wananchi wa Mkoa huo kushuhudia kutia nanga kwa meli ya Sea Star huko katika bandari ya Wete. MMILIKI wa kampuni ya Sea Feries ‘Turki’ akizungumza na viongozi mbali mbali na wananchi waliofika bandarini Wete kupokea meli ya kampuni hiyo, MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman akizingumza na wananchi mbali mbali wa Mkoa huo baada ya meli ya kampuni ya Sea Feries Sea Star 1 kufunga gati huko Wete. MKUU
Fursa: Ufadhili katika masomo vyuo vikuu “Scholarship” nchini Uturuki

Fursa: Ufadhili katika masomo vyuo vikuu “Scholarship” nchini Uturuki

Updates
Uongozi wa waturuki wanaoishi nje ya nchi na jamii zinazohusiana (YTB) umetangaza kuanza kupokea maombi ya wanafunzi wa kimataifa katika elimu ya vyuo vikuu wanaotaka kufanya mafunzo yao Uturuki. Maombi ya udhamini  kwa mwaka 2019 yameanza kupokelewa. Udhamini unaotolewa na Uturuki kupitia YTB unawawezesha wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali kudhaminiwa katika masomo ya fani mbalimbali katika vyuo vikuu maarufu nchini Uturuki, Ni aina ya Ufadhili ambayo inajulikana kwa kuwa na  ushindani mkubwa. Maombi ya ufadhili wa Uturuki kwa mwaka 2019, yameanza kupokelewa Januari 15 mwisho wa kupokea maombi ni Februari 20. Kufanya maombi ni bure. Maombi kwa njia ya posta au kwa njia ya mkono hayatakubaliwa. Wanafunzi wote wanaotaka ufadhili kwa daraja...
error: Content is protected !!