Erdogan aitaka Saudia imfichue aliyetoa agizo la kuua Jamal Khashoggi

Erdogan aitaka Saudia imfichue aliyetoa agizo la kuua Jamal Khashoggi

Kimataifa, Siasa
Kwa mara nyingine tena Rais Recep Tayyib Erdogan wa Uturuki ameitaka Saudi Arabia imfichue mtu ambaye alitoa amri ya kuuawa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Aal-Saud. Erdogan amekariri hayo leo akihutubia wanachama wa chama chake tawala cha Justice and Development Party (AKP) mjini Ankara na kuongeza kuwa, Riyadh inapaswa kuweka wazi jina la mtu aliyewapa agizo watu 15 walioenda Istanbul kufanya mauaji hayo. Rais wa Uturuki amehoji, "kwa nini raia hao 15 wa Saudia walikutana Istanbul? Nani aliwapa maagizo hayo? Kwa nini ubalozi mdogo wa Istanbul haukufunguliwa mara moja baada ya kuuawa Khashoggi bali siku kadhaa baadaye? Kadhalika ameitaka Saudia ifichue uliko mwili wa Khashoggi sanjari na kumfichua raia wa Uturuki ambaye Riyadh inadai ilimkabi
Jamal Khashoggi: Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump

Jamal Khashoggi: Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump

Kimataifa
Mchumba wa mwanahabari wa Saudia aliyeuawa Jamal Khashoggi anasema amesusia mwaliko wa rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwa madai kiongozi huyo wa haijaonesha nia ya kutaka kujua ukweli kuhusu mauaji hayo ya kikatili. Hatice Cengiz amekiambia kituo kimoja cha Televisheni nchini Uturuki kwamba mwaliko huo unalenga kubadili maoni ya Wamarekani Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul wiki tatu zilizopita. Riyadh imekanusha madai ya kuhusishwa kwa familia ya kifalme katika mauaji hayo na badala yake imelaumu watu iliyowataja kuwa''maajenti wakatili'' Katika mahojiano ya kusikitisha katika televisheni bi Cengiz alielezea jinsi mchumba wake alivyotoweka baada ya kuingia ubalozi wa Saudia mjini Istanbul. Anasema ''Kama ni...
Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kuwachoma visu watoto wa checkechea 14 katika eneo la Chongching nchini China

Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kuwachoma visu watoto wa checkechea 14 katika eneo la Chongching nchini China

Kimataifa
Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kuwachoma visu watoto wa checkechea 14 katika eneo la Chongching nchini China. Kwa mujibu wa habari,watoto hao wa shule ya chekechea inayojulikana kwa jina la “Yudong Şinşıci”walikuwa wakifanya mazoezi wakati mshambuliaji huyo alipovamia na kuwashambulia kwa kisu. Majeruhi wamefikishwa hospitalini. Mshambuliaji ni mwanamke wa miaka 39 anaejulikana kwa jina la Liu. Mpaka hivi sasa sababu ya shambulizi hilo haijajulikana na uchunguzi unaendelea.
Sahle-Work Zewde: Rais mpya wa Ethiopia asiye na ‘meno’

Sahle-Work Zewde: Rais mpya wa Ethiopia asiye na ‘meno’

Kimataifa, Siasa
Taarifa za Ethiopia kumchagua rais wa kwanza mwanamke zimepokelewa kwa shangwe kote barani Afrika, lakini swali ni; rais huyo ana mamlaka gani? Katika Jamuhuri nyingi duniani cheo cha rais kinashikilia mamlaka yote ya kisiasa na kidola. Jina la rais linawakilisha nguvu na uwezo wa kufanya maamuzi ya mwisho kwa mujibu wa katiba. Changamoto kubwa ya kisiasa duniani na hususan Afrika ni kuwaamini na kuwachagua wanawake katika nafasi kuu za kiuongozi. Na pale inapotokea mwanamke kuchaguliwa katika ofisi kuu ya nchi moja bara zima hushangilia na kupigia mfano. Kuchaguliwa Bi Sahle-Work Zewde na wabunge kuwa rais wa Ethiopia ni habari nzuri katika harakati za kuwainua wanawake wa Afrika, lakini wengi walioshangilia ushindi wake nje ya Ethiopia hawafahamu ukomo wa mamlaka yake. Wengi ...
Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya: Kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu si uhuru wa kujieleza

Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya: Kumvunjia heshima Mtume wa Uislamu si uhuru wa kujieleza

Jamii
Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya imehukumu kwamba, kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) si sehemu ya uhuru wa kujieleza. Mahakama hiyo imesema kuwa, uamuzi uliotolewa na mahakama moja ya Austria iliyomhukumu mwanamke mmoja kwamba amemvunjia heshima Mtume wa Uislamu haukukiuka haki ya kijieleza na si kinyume na kifungu nambari kumi cha hati ya haki za binadamu ya Umoja wa Ulaya. Uamuzi huo wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya ulitolewa jana Alkhamisi ukiunga mkono hukumu iliyotolewa na mahakama moja ya Austria dhidi ya mwanamke aliyehukumiwa kulipa faini ya Euro 480 na gharama za kesi hiyo kwa kupatikana na hatia ya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw). Uamuzi wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya umesema: Mahakama za Austria zimepima kwa umakini mkubwa baina ya hak...
error: Content is protected !!