Timu ya Mwenge Pemba yasema, itaabani kwa madeni ya mwaka jana

Timu ya Mwenge Pemba yasema, itaabani kwa madeni ya mwaka jana

Michezo
WAKONGWE wa soka kisiwani Pemba wenye maskani yao Wete Pemba, Timu ya Mwenge imesema imeondosha matumaini ya kufanya maandalizi ya ligi kwa msimu wa 2018/2019. Kocha wa timu hiyo Mussa Salum Bajaka, alisema sababu kubwa ya kuondosha kwa matumaini kwao, kutokana na bado madeni waliokopa kwa ajili ya kuihudumia timu kwa msimu uliomalizika hajayalipwa. Alisema fedha hizo walikopa kwa kuihudumia timu yao mahitaji mbali mbali, hivyo ni vigumu kuiweka timu kambini kwa sasa, ikiwa madeni ya mwaka jana bado wanayo. “Sisi bado hatujafanya uhamisho wa mchezaji yoyote wala kuacha mchezaji, msimu huu ni mgumu kwetu tumemaliza mashindano mwezi uliopita wala hatujajua chakufanya,”alisema. Alisema kutokana na hali hiyo hawawezi kuwa na maandalizi yoyote kwa msimu huu, kwani hajafanya usaj
Seneta Collins atangaza kumpigia kura Kavanaugh

Seneta Collins atangaza kumpigia kura Kavanaugh

Kimataifa, Siasa
Seneta Susan Collins wa Marekani, Mrepublikan ambaye anachukuliwa kuwa mwenye kura ya kubadilisha matokeo kati ya wawakilishi watakao amua uteuzi wa Jaji Brett Kavanaugh kuingia Mahakama ya Juu Marekani, ametangaza kuwa atampigia kura mteule huyu. Kura ya kumthibitisha Jaji Kavanaugh inaweza kupigwa mapema Jumamosi. Collins amesema kukosekana ushahidi kwa tuhuma dhidi ya Kavanaugh ndio sababu ya kumuunga mkono. Lakini ameongeza kuwa uamuzi wake isichukuliwe kwamba anakanusha umuhimu wa madai ya unyanyasaji wa kingono. “Kila mtu au mwanamke ambaye anashtaki juu ya udhalilishaji wa kingono anahaki ya kusikilizwa na kuwekewa heshima yake,” amesema. Kura ya Collins ya ndiyo inafanya kuthibitishwa kwa Kavanaugh kuwa na uwezekano mkubwa. Iwapo kura ya Seneta Mdemokrat
Teknolojia ya Ultrasound na uzazi: Kuna madhara au manufaa yoyote kufahamu jinsia ya mtoto kabla hajazaliwa?

Teknolojia ya Ultrasound na uzazi: Kuna madhara au manufaa yoyote kufahamu jinsia ya mtoto kabla hajazaliwa?

Afya
Kufahamu jinsia ya mtoto akiwa tumboni kwa kutumia teknolojia ni mtindo ambao umekuwa ukipata umaarufu, lakini pia kuzua mdahalo mkubwa hasa katika nchini za Kiafrika. Kila mtu na imani yake, baadhi ya kina mama huamini kujua jinsia ya mtoto mapema ni kutafuta mikosi. Lakini wengine huamini ni jambo jema kwani inakupa fursa ya kujiandaa na vitu muhimu vya mtoto, kwa mfano mavazi na pia jina la mtoto. Wanawake wa kisasa hupendelea zaidi kujua jinsia ili waweze kuandaa sherehe maalumu inayoitwa Baby Shower. Katika sherehe hii akina mama hawa huweka wazi jinsia ya mtoto kwa kupamba mandari ya pinki kwa mtoto wa kike na buluu kwa mtoto wa kiume. Baadhi hupokea zawadi zenye rangi mbali mbali zisizobagua jinsia mfano rangi nyeupe, kijivu, njano na hata nyeusi na nyekundu. Si wote ...
Wanaume wavalia kama Wanawake kazini, Meneja wao aeleza sababu ya kuvaa hivyo

Wanaume wavalia kama Wanawake kazini, Meneja wao aeleza sababu ya kuvaa hivyo

Kimataifa
Ukizitazama picha hizi, unaweza ukadhani unawatazama wanamitindo, au ukadhani kuna wanawake kwenye picha hii. Lakini wote ni wanaume, na si wanamitindo pia. Ni wafanyakazi wa kampuni moja nchini Kenya walioamua kuvalia kama wanawake kazini kama sehemu ya maadhimisho ya kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya kiafya ya wanawake, na zaidi saratani Oktoba ukiwa mwezi wa kuhamasisha kuhusu saratani ya matiti. Picha zao zimesambazwa sana mtandaoni Kenya, baadhi wakiwapongeza na wengine kukosoa hatua hiyo. Walioshiriki walikuwa wafanyakazi wa kiume wenye vyeo mbalimbali katika kampuni hiyo, akiwemo afisa mkuu mtendaji Guy Jack. Meneja wa huduma kwa wateja Stella Kamau ameambia BBC kwamba wazo la wanaume kuvalia mavazi ya kike kazini liliibuka katika moja ya vikao vilivyokuwa vikijadi...
TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR

TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR

Michezo
Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limeteua kamati mpya ndogo ya wajumbe 10 watakao simamia soka la Zanzibar kwa muda mfupi. Akizugumza na Wandishi wa Habari katika Ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan Raisi wa Shirikisho hilo Wallace Karia amesema kamati hiyo itakuwa na jukumu la kusimamia upatikanaji wa Katiba ya ZFA, kushughulikia shughuli zote za ZFA za Kikatiba pamoja na kutayarisha Uchaguzi mpya kwaajili ya kupatikana viongozi wapya wa ZFA. Karia amesema kamati hiyo wameiyunda baada ya vikao vya muda mrefu baina ya pande zote na kupata muafaka wa TFF kuunda kamati hiyo ambayo itafanya kazi zake hadi Novemba 30 mwaka huu. Kuhusu suala la kamati ya iliounda mrajisi wa vyama vya michezo Karia amesema kamati hiyo kwa sasa haitofanya kazi tena baada ya TFF kuteuwa kamati ...
error: Content is protected !!