Pingamizi la Myanmar kwa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kizazi ya Waislamu Warohingya

Pingamizi la Myanmar kwa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kizazi ya Waislamu Warohingya

Jamii, Kimataifa
Mkuu wa majeshi ya Myanmar ametangaza kuwa, Umoja wa Mataifa hauna haki ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo kupitia uchunguzi kuhusiana na wakazi wa jimbo la Rakhine la magharibi mwa nchi hiyo. Jenerali Min Aung Hlaing ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutekeleza mashambulio ya kikatili na ya mauaji ya kizazi dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya amesema kuwa kwamba, sio Umoja wa Mataifa, wala nchi au kundi lolote lile amballo lina haki ya kuingilia mambo ya ndani ya Myanmar au kuchukua maamuzi kuhusiana na mamlaka ya kujitawala nchi nyingine. Hii ni radiamali ya kwanza ya viongozi wa Myanmar tangu kutolewa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na nchi hiyo. Katika ripoti yake hiyo, Umoja wa Mataifa ulilinyooshea kidole jeshi la Myanmar na kulitangaza kuwa, limefanya mauaji ya k
Baada ya kimya cha muda mrefu Marekani yakiri, kumefanyika jina kubwa dhidi ya Waislamu, Myanmar

Baada ya kimya cha muda mrefu Marekani yakiri, kumefanyika jina kubwa dhidi ya Waislamu, Myanmar

Jamii, Kimataifa
Baada ya kunyamaza kimya kwa muda mrefu mbele ya jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar, hatimaye Marekani imetoa ripoti ikisisitiza kuuwa jeshi la nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia limefanya jinai na uhalifu wa kupanga na ulioratibiwa dhidi ya jamii hiyo. Ripoti hiyo imesema kuwa: Vurugu za hivi karibuni huko kaskazini mwa jimbo la Rakhine nchini Myanmar zilikuwa kali, kubwa na pana na inaonekana kuwa zilifanyika kwa lengo la kutisha watu na kuwafukuza wakazi wa Rohingya katika makazi yao. " Ripoti hiyo ya Marekani imesema jeshi la Myanmar lilifanya mashambulizi ya makusudi yaliyojumuisha mauaji, kubaka wanawake kwa umati na ukatili mwingine dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya. Ripoti hiyo imetayarishwa baada ya k...
Chama kikuu cha upinzani Uganda -FDC-chagawanyika

Chama kikuu cha upinzani Uganda -FDC-chagawanyika

Siasa
Forum for Democratic Change party president Mugisha Muntu Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda kimegawanyika kufuatia tangazo la aliyekuwa rais wa chama hicho Mugisha Muntu kwamba ameamua kuondoka katika chama hicho baada ya mazungumzo na wafuasi wa chama na juhudi za maridhiano ndani ya chama kushindwa kufaulu. Mugisha Muntu, ambaye alikuwa rais wa chama hicho ametangaza uamuzi huo baada ya kikao na uongozi chini ya rais wa sasa Patrick Amuriat. Hata hivyo, Muntu hajatangaza mwelekeo wake mpya, lakini tayari kuna minong’ono kati ya raia wa Uganda kwamba anaelekea kushirikiana na mbunge Bobi Wine katika safari mpya ya kisiasa. Uamuzi wake unafuatia miezi saba ya majadiliano na wanachama wa FDC kote nchini Uganda baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata wa chama hicho, na kuacha ny
Goli la ugenini lapelekwa mkutano mkuu UEFA

Goli la ugenini lapelekwa mkutano mkuu UEFA

Michezo
PARIS, Ufaransa SHIRIKISHO la Soka la Ulaya (UEFA) limekubali kijadili mapendekezo yaliyotolewa na umoja wa mameneja wa klabu kubwa barani humo ya kufuta sheria ya bao la ugenini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi ya Europa kuanzia msimu ujao. Kaimu Katibu Mkuu wa UEFA, Giorgio Marchetti, amethibitisha pendekezo hilo kuingizwa kwenye ajenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano mkuu, utakaofanyika baadaye mwaka huu. “Pendekezo lao tumelipokea na kwa bahati nzuri litakuwa ni sehemu ya ajenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano mkuu, tuwaachie wahusika na kuona kama watapitisha pendekezo la kufutwa kwa sheria hiyo”, alisema,Marchetti. “Wao wanaamini ni sheria kandamizi kwa timu ambayo hutolewa mashindanoni kwa bao la ugenini, lakini bado ni mapendekezo yao, tumeyaheshimu
Uswiss yakataa maombi ya Roman Abramovich

Uswiss yakataa maombi ya Roman Abramovich

Kimataifa, Michezo
Roman Abramovich mmiliki wa timu ya Chelsea Mamlaka nchini Switzerland imetupilia mbali maombi ya kuishi nchini humo kutoka kwa bilionea wa Kirusi Roman Abramovich. Bilionea huyo ni mmiliki wa klabu ya mpira ya Chelsea ambaye alituma maombi yake ya kutaka kuishi maeneo ya mapumziko ya Alpes ya Verbier, ambapo awali alikubaliwa , lakini polisi wa shirikisho la Uswisi walitoa sababu ya kukataa ombi hilo kuwa wanahisi Abramovich anaweza kuhatarisha usalama na hivyo basi ombi lake likatupiliwa mbali. Mpaka sasa hakuna ushahidi wowote wa kihalifu alioutenda, na mwanasheria wa Abramovich amesema kwamba madai hayo wanayomshukia yote ni ya uongo. Abramovich anatuhumiwa kwa uhalifu wa kutakatisha fedha na makosa mengine ya jinai yote hayo bado hayajathibitishwa, lakini mamlaka nchini Uswis...
error: Content is protected !!