ZAECA yakamilisha uchunguzi upotevu wa 1.6bn/

ZAECA yakamilisha uchunguzi upotevu wa 1.6bn/

Biashara & Uchumi, Nyumbani
MKURUGENZI wa Mamkala ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), Mussa Haji amesema majalada ya upotevu wa fedha za serikali zinazofikia shilingi bilioni 1.6, wakati wowote kutoka sasa yatakabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka. Tuhuma za upotevu wa fedha hizo zinawakabili baadhi ya wahasibu wa taasisi za umma na maofisa kutoka wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar. Alisema ZAECA kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya uchunguzi, vimekamilisha na kujiridisha na uchunguzi walioufanya na kwamba hatua iliyobaki ni kuyafikisha majalada hayo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP) kwa hatua nyengine za kisheria. Mkurugenzi huyo alieleza hayo wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Vuga, mjini Zanzibar ambapo alisema katika uchunguzi huo uliwashirikisha na vyombo vyengine ...
Koffi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi

Koffi Annan kuzikwa Ghana, Alhamisi

Kimataifa
Mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana. Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa. Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi. Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi. Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa. Akiwa na Malkia wa Uingereza Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu kati...
“Mtu anaogopa kuongea Kiswahili, haya ni maajabu kweli”- JPM

“Mtu anaogopa kuongea Kiswahili, haya ni maajabu kweli”- JPM

Mikoani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa amesikitishwa na Watanzania wanaoona aibu kuongea Kiswahili na kujilazimisha kuongea Kiingereza. Ameyasema hayo kwenye mkutano wake wa hadhara wilayani Meatu mkoani Simiyu na kutolea mfano Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA), Jacqueline Mahon ambaye amekuwa akitumia lugha ya Kiswahili. “Uzalendo wetu ni kulinda cha kwetu unaweza ukaona hapa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon, anatoka Ulaya na amekipiga Kiswahili vizuri tu lakini unakuta Mswahili wa Tanzania ambaye anatakiwa kuitangaza lugha yetu anaogopa anataka azungumze Kiingereza,”amesema rais Dkt. Magufuli Aidha, katika mkutano huo, Jacqueline amesema kuwa mikakati ya
Serikali imeshauriwa kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili kuongezeka kwa deni ili kuweza kufikia ufumbuzi juu ya sakata la ushuru wa asilimia 16 uliowekwa kwenye bidhaa za mafuta nchini Kenya.

Serikali imeshauriwa kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili kuongezeka kwa deni ili kuweza kufikia ufumbuzi juu ya sakata la ushuru wa asilimia 16 uliowekwa kwenye bidhaa za mafuta nchini Kenya.

Biashara & Uchumi
Serikali imeshauriwa kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili kuongezeka kwa deni ili kuweza kufikia ufumbuzi juu ya sakata la ushuru wa asilimia 16 uliowekwa kwenye bidhaa za mafuta nchini Kenya. Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA anaripoti kuwa deni hilo hivi sasa limefikia takriban shilingi trilioni tano ambazo ni sawa na dola za Marekani bilioni 49. Akitoa ushauri huo wa serikali kufanya mazungumzo Jumatatu, Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa mikopo hii kutoka mataifa ya kigeni ni mzigo mkubwa kwa raia wa Kenya. Wakati huohuo mjadala unaendelea Kenya, wananchi wakinong’onezana kuhusu deni la nchi kutoka mataifa ya Kigeni, hususan Uchina na iwapo Kenya inajiingiza katika mtego wa madeni ya China. Akiwa kwenye mkutano kati ya viongozi wa bara la Afr
error: Content is protected !!