Palestina: Marekani ni mlinda maslahi ya Israel

Palestina: Marekani ni mlinda maslahi ya Israel

Kimataifa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amesema kuhusiana na kufungwa ofisi ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) nchini Marekani kwamba hatua hiyo imethibitisha kwa mara nyingine kuwa Washington ni mwakilishi pekee wa Israel na mlinda maslahi ya utawala huo wa Kizayuni. Waziri wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameongeza kuwa: hatua ya Marekani ya kuifunga ofisi ya PLO imethibitisha kwa mara nyingine upeo wa kujitolea nchi hiyo katika kulinda maslahi ya Israel na kuonyesha kwamba iko tayari kwa hali yoyote ile kuuhami utawala wa Tel Aviv. Riyadh al-Maliki aidha ameitaka serikali ya Palestina iandae faili la kesi ya kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina na kulifikisha kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Jengo la ofisi ya PLO m
Wafanyabiashara Watakiwa Kutumia Mawakala Waliothibitishwa na TRA Kupata Karatasi za Risiti.

Wafanyabiashara Watakiwa Kutumia Mawakala Waliothibitishwa na TRA Kupata Karatasi za Risiti.

Biashara & Uchumi, Mikoani
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb). Na.Peter Haule. Serikali imetatua tatizo la kuwepo kwa karatasi za risiti  zinazofutika maandishi zinazotolewa na Mashine za Kielektroniki za kutolea Risiti (EFDs)  kwa kuwataka wafanyabiashara wote kununua karatasi hizo kwa mawakala waliothibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Mussa Bakari Mbarouk, aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu risiti zinazotolewa na Mashine za EFDs kufutika maandishi kwa muda mfupi na muda ambao utatolewa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kurekebisha hali hiyo. Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serika
WIZARA ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kupitia Idara ya Ajira imewataka wananchi wanaopata fursa ya kwenda kufanyakazi nje ya nchi kuhakikisha kuwa wanapitia katika wizara hiyo ili kuepusha vitendo vya ukatili na udhalilishaji wanavyofanyiwa.

WIZARA ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kupitia Idara ya Ajira imewataka wananchi wanaopata fursa ya kwenda kufanyakazi nje ya nchi kuhakikisha kuwa wanapitia katika wizara hiyo ili kuepusha vitendo vya ukatili na udhalilishaji wanavyofanyiwa.

Biashara & Uchumi
WIZARA ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kupitia Idara ya Ajira imewataka wananchi wanaopata fursa ya kwenda kufanyakazi nje ya nchi kuhakikisha kuwa wanapitia katika wizara hiyo ili kuepusha vitendo vya ukatili na udhalilishaji wanavyofanyiwa. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ajira, Ali Suleiman Ameir, wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake, Mwanakwerekwe. Alisema, kijana hatoondoka kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanyakazi bila ya kufuata taratibu, ambapo kama wizara inatakiwa kujua aina ya kazi ambayo atakwenda kufanya, lakini pia waweze kuona mkataba wa ajira baina ya wakala wa ajira wa nje ya nchi na wa ndani. Aidha alisema Wizara inatakiwa pia kujua mkataba huo umewaunganisha katika kitu gani na ni aina gani ya kazi amb...
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu CCM Mhe. Simai Mohammed Said Amewaasa Watoto Kusoma Quran Ili Iwajenge Kimaadili

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu CCM Mhe. Simai Mohammed Said Amewaasa Watoto Kusoma Quran Ili Iwajenge Kimaadili

Jamii
Na Salum Vuai JAMII katika Wilaya ya Kati, imehimizwa kuwasimamia vyema watoto na kuhakikisha wanasoma vizuri elimu zote, dini na dunia. Akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Kuran kwa madrasa za kanda ya Bungi katika jimbo la Tunguu, Mwakilishi wa jimbo hilo Simai Mohammed Said, amesema elimu ya dini ndio dira ya kuwaongoa watoto wa Kizanzibari. Amesema vitendo vya udhalilishaji vilivyokithiri nchini, vinaweza kudhibitiwa iwapo kila mzazi atabeba kikamilifu dhima ya uchunga wa familia kwa ushirikiano na wanajamii wote. Simai alieleza kufurahishwa na utaratibu wa kuandaa mashindano hayo ya kuhifadhi kitabu kitatakatifu cha Mwenyezi Mungu, akisema hicho cha kwanza kwani kimebeba mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu. “Usomi wowote unaendana na kusoma vitabu vya aina
error: Content is protected !!