
Shamsi ashauri wakandarasi kuacha tamaa
MWENYEKITI wa Kamati teule ya kuchunguza majengo ya skuli 19 za
sekondari, Rashid Makame Shamsi, amewashauri wakandarasi wanaopewa kazi
na serikali kuacha tamaa na maslahi binafsi badala yake wajali maslaji
ya wananchi.
Aliyasema hayo wakati akifanya majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo, katika kikao cha baraza la wawakilishi,Chukwani.
Alisema kampuni nyingi zinazopewa kazi na serikali zinafanya ubadhirifu jambo ambalo linasababisha hasara kwa serikali.
Hata hivyo, alishauri wizara kuwachukulia hatua wote waliobainika kuhusika katika ubadhirifu.
Alisema serikali inawaamini wakandarasi lakini wameshindwa
kujiaminisha kwani wanavunja masharti ya mikataba jambo ambalo
linarejesha nyuma maendeleo ya nchi.
Sambamba na hayo, kamati hiyo imependekeza wakala wa ...