Magaidi wa ISIS walijizatiti vilivyo Iraq, maghala mengine ya kemikali yagunduliwa Salahuddin, al Anbar

Magaidi wa ISIS walijizatiti vilivyo Iraq, maghala mengine ya kemikali yagunduliwa Salahuddin, al Anbar

Kimataifa
Vikosi vya usalama vya Iraq vimegundua maghala mengine ya silaha za kemikali za genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika mikoa ya Salahuddin na al Anbar, jambo ambalo linathibitisha ni kiasi gani magaidi hao walikuwa wamejizatiti kwa silaha za kila namna hasa za kemikali na za mauaji ya umati. Vikosi vya kulinda usalama vya Iraq vinaendelea na operesheni zao za kusafisha mabaki na silaha za magaidi wa Daesh na kila leo vinagundua maficho ya silaha za wakufurishaji hao. Kituo cha taarifa za kiusalama cha Iraq kimetoa taarifa mbili na kusema kuwa, askari wa nchi hiyo wamefanikiwa kugundua maghala mengine ya mada za kemikali katika maeneo ya mikoa iliyokombolewa ya al Anbar na Salahuddin. Wakati fulani mikoa hiyo ilikuwa ni ngome kuu za genge la ukufurishaji la Daesh huko Iraq. Kanali...
Rushwa ya wafugaji yaua askari wawili kigoma

Rushwa ya wafugaji yaua askari wawili kigoma

Mikoani
Siri imefichuka kuwa vurugu iliyoibuka Oktoba 18 na kusababisha vifo vya askari wawili katika kijiji cha Mpeta mkoani Kigoma zimetokana na wafugaji kuchoka kutoa rushwa ili wasisumbuliwe na kufukuzwa katika eneo hilo. Vurugu hizo zilitokea katika kitongoji cha Mwandulubantu ambacho kinadaiwa kuvamiwa na wafugaji na kuanzisha makazi. Eneo hilo linadaiwa kuwa ni hifadhi na haliruhusiwi kutumika kwa shughuli za kibinadamu bila idhini ya Serikali. Akizungumza na Mwananchi juzi, mmoja wa wafugaji hao alisema awali kulikuwa na wafugaji wachache waliovamia na baada ya kuweka makazi wakaongezeka ambapo kwa sasa wanakadiriwa kufikia 1,500. “Chanzo cha vurugu ni wafugaji kuchoka kuliwa fedha zao kwa sababu kuna baadhi ya watu wanakuja kuomba pesa eti wapeleke kwa wakubwa ili wafugaji
Erdogan aitaka Saudia imfichue aliyetoa agizo la kuua Jamal Khashoggi

Erdogan aitaka Saudia imfichue aliyetoa agizo la kuua Jamal Khashoggi

Kimataifa, Siasa
Kwa mara nyingine tena Rais Recep Tayyib Erdogan wa Uturuki ameitaka Saudi Arabia imfichue mtu ambaye alitoa amri ya kuuawa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Aal-Saud. Erdogan amekariri hayo leo akihutubia wanachama wa chama chake tawala cha Justice and Development Party (AKP) mjini Ankara na kuongeza kuwa, Riyadh inapaswa kuweka wazi jina la mtu aliyewapa agizo watu 15 walioenda Istanbul kufanya mauaji hayo. Rais wa Uturuki amehoji, "kwa nini raia hao 15 wa Saudia walikutana Istanbul? Nani aliwapa maagizo hayo? Kwa nini ubalozi mdogo wa Istanbul haukufunguliwa mara moja baada ya kuuawa Khashoggi bali siku kadhaa baadaye? Kadhalika ameitaka Saudia ifichue uliko mwili wa Khashoggi sanjari na kumfichua raia wa Uturuki ambaye Riyadh inadai ilimkabi
Jamal Khashoggi: Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump

Jamal Khashoggi: Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump

Kimataifa
Mchumba wa mwanahabari wa Saudia aliyeuawa Jamal Khashoggi anasema amesusia mwaliko wa rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwa madai kiongozi huyo wa haijaonesha nia ya kutaka kujua ukweli kuhusu mauaji hayo ya kikatili. Hatice Cengiz amekiambia kituo kimoja cha Televisheni nchini Uturuki kwamba mwaliko huo unalenga kubadili maoni ya Wamarekani Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul wiki tatu zilizopita. Riyadh imekanusha madai ya kuhusishwa kwa familia ya kifalme katika mauaji hayo na badala yake imelaumu watu iliyowataja kuwa''maajenti wakatili'' Katika mahojiano ya kusikitisha katika televisheni bi Cengiz alielezea jinsi mchumba wake alivyotoweka baada ya kuingia ubalozi wa Saudia mjini Istanbul. Anasema ''Kama ni...
Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kuwachoma visu watoto wa checkechea 14 katika eneo la Chongching nchini China

Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kuwachoma visu watoto wa checkechea 14 katika eneo la Chongching nchini China

Kimataifa
Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kuwachoma visu watoto wa checkechea 14 katika eneo la Chongching nchini China. Kwa mujibu wa habari,watoto hao wa shule ya chekechea inayojulikana kwa jina la “Yudong Şinşıci”walikuwa wakifanya mazoezi wakati mshambuliaji huyo alipovamia na kuwashambulia kwa kisu. Majeruhi wamefikishwa hospitalini. Mshambuliaji ni mwanamke wa miaka 39 anaejulikana kwa jina la Liu. Mpaka hivi sasa sababu ya shambulizi hilo haijajulikana na uchunguzi unaendelea.
error: Content is protected !!