DC JOKATE MWEGELO AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MUHOGO KIJIJI CHA KITANGA, KISARAWE

DC JOKATE MWEGELO AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MUHOGO KIJIJI CHA KITANGA, KISARAWE

Mikoani
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amepongeza jitihada za akinamama katika kubuni miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa Serikali iko tayari kuunga mkono jitihada zao, na hasa katika miradi ya kilimo ambayo inaleta uhakika wa chakula. DC Mwegelo amesema hayo leo, Jumamosi, Septemba 15, 2018 wakati akiweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe, ambacho kinamilikiwa na akinamama wapatao 30 wanaoongozwa na Ofisa Kilimo mstaafu, mama Abia Magembe. Mkuu huyo wa wilaya aliweka jiwe hilo la msingi kwa niaba ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe. Alisema anapongeza jitihada kubwa zilizofanywa na akinamama hao siyo tu katika kubuni miradi ya maendel...
Fuat Oktay: “Uturuki yaanza kupiga hatua katika sekta ya teknolojia”

Fuat Oktay: “Uturuki yaanza kupiga hatua katika sekta ya teknolojia”

Teknolojia
Fuat Oktay, makamu wa rais wa Uturuki amefahamisha kuwa Uturuki yapiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia . Hayo makamu wa rais ameyazungumza  baada ya Uturuki  kuonesha kuwa imefanya mabadiliko makubwa  na kupiga hatua katika uundaji wa vifaa vya anga vya kivita. Sekta ya ulinzi nchini Uturuki  imepiga  hatua kwa kuunda kwa vifaa vipya  vya anga vya kivita. Uturuki iliandaa maonesho  ya vifaa vya kivita vya anga mjini Istanbul TEKNOFEST kuanzia Alkhamis hadi Jumapili. Uturuki imeanza kuona matunda ya juhudi ambazo wanasayansi  wamejitolea ili kuakikisha kuwa sekta ya ulinzi Uturuki inakuwa imara. Makamu wa rais wa Uturuki Fuat Oktay amepongeza  tamasha hilo la TEKNOFEST  na kutoa pongezi kwa wote wale ambao  walitoa mchango wao ili kufaanikisha mradi huo ambao l
Aliyedhaniwa kuwa Mchawi azusha Tafrani Kwarara Zanzibar

Aliyedhaniwa kuwa Mchawi azusha Tafrani Kwarara Zanzibar

Jamii, Nyumbani
Mzee mmoja anaekadiriwa kuwa na miaka 60 amezusha tafrani kubwa huko Kwarara maduka sita Wilaya ya Magharibi B Unguja baada ya kuomba choo na kuhisiwa anafanya mambo ya ushirikina katika choo hicho. Tukio hilo limetokea jana Septemba 23 majira ya saa 10 jioni. Akizungumza na Zanzibar24 mama mwenye nyumba hiyo amesema kuwa, Bibi  huyo alikwenda kuomba choo nyumbani hapo majira ya saa 10 jioni na kuruhusiwa kwenda kufanya haja yake, lakini alikawia kutoka chooni hapo na hatimae mama mwenye nyumba kumchunguza kwa kumchungulia na kumbaini anafanya shughuli zisizo za kawaida chooni hapo. “Nilikua nachoma mikate baada ya kumaliza kuchoma mikate nilikaa muda wa nusu saa sisikii maji chooni kitendo hicho kilinishangaza na kunitia hofu nilikwenda nikafungua pazia kwakumtizama nika muona k
Serikali ya Benin yaondoa kodi ya mitandao ya kijamii

Serikali ya Benin yaondoa kodi ya mitandao ya kijamii

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa
Serikali  ya Benin yaondoa kodi  iliokuwa imewekwa  kwa ajili ya mitandao ya kijamii. Serikali ya Benin yachukuwa aumuzi wa  kuondoa kodi iliokuwa imewekwa kwa ajili ya mitandao ya kijamii. Sheria hiyo kuhusu mitandao ya kijamii iliwekwa  Julai. Raia nchini humo waliandamana kupinga sheria hiyo na kuishinikiza  serikali kuondoa sheria hiyo. Rais wa Benin Patrice Talon  na wizara inayohusika na mitandao wamefahamisha katika kurasa zao  kuwa sheria hiyo ya kutoza kodi  mitandao ya kijamii imeondolewa.
Serikali kujenga kituo kipya cha gari za abiria Mkokotoni

Serikali kujenga kituo kipya cha gari za abiria Mkokotoni

Nyumbani
SERIKALI imesema itakihamisha kituo cha gari za abiria za Mkokotoni na Donge, kilichopo mbele ya soko la Mkokotoni na kujenga chengine kipya. Baada ya kujengwa, kituo hicho cha zamani kitatumiwa kwa wasafiri wanaokwenda kisiwa cha Tumbatu. Mratibu wa ujenzi wa barabara ya Chuini-Mkokotoni, Pete Jumanne Magese, alisema hayo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mustafa Aboud Jumbe, aliefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara hiyo. Alisema serikali itajenga kituo kipya kutokana na cha sasa kuwa kidogo na kuvamiwa na wafanyabiashara. Nao wananchi ambao watapisha ujenzi wa kituo hicho,walisema wako tayari kuhama endapo watalipwa fidia. Makame Haji Makame, mmoja ya wananchi hao, alisema yuko tayari kuhama kwa sababu kituo hicho kitatu...
error: Content is protected !!