Google: wafanyakazi 48 wafutwa kazi kutokana na unyanyasaji wa kingono

Google: wafanyakazi 48 wafutwa kazi kutokana na unyanyasaji wa kingono

Biashara & Uchumi, Teknolojia
Google imewafuta kazi watu 48 wakiwemo maafisa 13 wakuu kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kingono tangu 2016. Katika barua kwa wafanyakazi wake, mkurugenzi mmkuu mtendaji Sundar Pichai amesema kampuni hiyo kubwa ya teknolojia inachukua 'msimamo mkali' dhidi ya tabia zisizo sawa. Barua hiyo inafuata ripoti ya New York Times kwamba muasisi wa mfumo wa Android Andy Rubin alipokea $90m kama kititia cha kuondoka licha ya kukabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu. Msemaji wa Bwana Rubin alikana tuhuma hizo, gazeti hilo limesema. Sam Singer amesema Bwana Rubin aliamua kuondoka Google mnamo 2014 kuanzisha kampuni yake ya teknolojia kwa jina Playground. 'Aliagwa kama shujaa' wakati alipoondoka, gazeti hilo linasema. Barua ya Pichai inasema ripoti ya New York Times ni "ngumu kuis...
Mahmoud akabidhi zawadi kwa ‘Siti and the band’

Mahmoud akabidhi zawadi kwa ‘Siti and the band’

Nyumbani
WAZIRI wa Habari, Utalii, Utamaduni na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabiti Kombo, amekabidhi zawadi kwa kikundi cha ‘Siti and the band’ baada ya kufanya vizuri katika Tamasha la Utalii lililofanyika hivi karibuni Unguja. Zawadi hizo ni muendelezo wa juhudi za rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein za kukiunga mkono kikundi hicho. Waziri Mahmoud alikikabidhi kikundi hicho pesa taslimu shilingi 5,000,000 zilizotolewa na mfadhili kutoka Oman Ahmed Suleiman, pamoja na dola 300. Akitoa nasaha zake mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, huko katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni, Waziri Mahmoud aliwaomba Wazanzibari wengine na wageni wanaokuja Zanzibar, kuendelea kuwaunga mkono vijana hao. Jambo walilolifanya katika tamasha la utalii ni jambo
Mwanaharakati auawa kwa kuchomwa kisu

Mwanaharakati auawa kwa kuchomwa kisu

Kimataifa
MWANAHARAKATI wa kisiasa nchi Kenya ameuawa kwa kuchomwa kisu  na mfanyabiashara mwenzake  katika mazingira ya kutatanisha usiku wa Jumatano. Hata hivyo imeelezwa kwamba mtuhumiwa alijisalimisha kwa polisi muda mfupi baada ya tukio hilo. Polisi alisema mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la  Joan Muthoni, alichomwa kisu cha  paja. Naibu Polisi Mkuu wa Nyeri , Paul Kuria alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kwamba mtu huyo kwa sasa anafanyiwa uchunguzi ili kuweza kuhukumiwa. “Alitangazwa kufariki baada ya kuwasili katika hospitali ya  Nyeri. M,tuhumiwa anafanyiwa upelelezi kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema. Marehemu alijulikana kutokana na uhamasishaji jamii na kampeni za kisiasa. Alikuwa akipendwa na viongozi wengi wakati wa kipindi cha kampeni....
Mwezi Bandia: China inaweza kuangaza mawingu usiku?

Mwezi Bandia: China inaweza kuangaza mawingu usiku?

Kimataifa, Teknolojia
Kampuni moja ya Uchina imetangaza mpango wake wa kubuni ''mwezi bandia" utakaoangaza miji usiku. Kwa mujibu wa gazeti la kitaifa la People's Daily, maafisa katika taasisi ya kibinafsi ya masuala ya anga za juu iliyoko mjini Chengdu inataka kuzindua "kituo cha satellite kitakachoangaza" ulimwengu. Mradi huo unatarajiwa kuzindiluwa ifikapo mwaka 2020, ambayo pia itakua na mwangaza wa haliya juu utakaochukua nafasi ya taa za barabarani. Mpango huo umevutia hisia mbali mbali kutoka kwa wanasayansi ambao wanahoji uwezekeno wa kufikiwa kwa mpango huo huku wengine wakiukejeli. Hakuna mengi yaliyoangaaziwa kuhusiana na mradi wenyewe - taarifa zilizotolewa kwa umma pia zinakinzana. Gazeti la People's Daily iliangzaia mradi huo kwa mara ya kwanza wiki iliyopita. Gazeti hilo lilimnu...
Watu 11 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa nchini Venezuela.

Watu 11 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa nchini Venezuela.

Kimataifa
Watu 11 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa nchini Venezuela. Maporomoko na mafuriko vimeendelea kusababisha vifo hasa katika maeneo ya Colombia,Venezuela,Panama. Utabiri wa hali ya hewa umeonyesha kuwa kuna dalili ya mvua kuendelea kunyesha mpaka katikakatika ya mwezi wa Desemba. Watu wengine watatu hawajulikani walipo. Mvua zimekuwa zikinyesha katika maeneo ya Merida, Lara, Delta, Sucre na Miranda.
error: Content is protected !!