Neymar awasilisha taarifa kwa polisi huku kampuni za matangazo zikianza kuvunja mkataba naye

Nyota wa Brazil Neymar alienda katika kituo cha polisi mjini Rio de Janeiro kuwasilisha taarifa kufuatia madai ya ubakaji , kulingana na wakili wake.

Nyota huyo amekana kumbaka Najila Trindade katika hoteli moja mjini Paris mnamo tarehe 15 mwezi Mei na kuwashukuru mashabiki wake nje ya kituo kwa usaidizi wao.

Bi Trindade aliwasilisha madai hayo Ijumaa iliopita akiambia runinga moja ya Brazil kwamba alikuwa anataka haki kutendeka.

Mastercard imesitisha matangazo yake na Neymar.

Kampuni hiyo ya kuchukua fedha kwa mkopo imesema kuwa itasitisha utumizi wa picha za nyota huyo, ambaye ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa cha fedha na anaichezea klabu ya PSG hadi pale tatizo hilo litakapotatuliwa.

Kampuni ya jezi za michezo Nike nayo ilikuwa imetangaza kwamba ina wasiwasi kuhusu madai ya ubakaji dhidi ya Neymar, ambaye inamfadhili.

Anasema kwamba wakati walipokutana na Neymar alikuwa mtu wa fujo ”mtu tofauti na yule niliyemjua katika ujumbe”.

Bi Trindade alikua amejiandaa kushiriki ngono lakini akataka watumie mipira ya kondomu. Anadai kwamba Neymar alikataa akaleta fujo na kumbaka.

Anasema kwamba alimwambia kuacha kufanya hivyo lakini akakataa.

SBT ilichapisha baadhi ya mahojiano hayo katika mtandao wa Twitter { kwa Kireno).

Ni nini kilichotokea katika kituo cha Polisi?

Neymar aliwasili katika kituo cha polisi kwa kutumia magongo baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu wakati wa mechi ya Brazil dhidi ya Qatar mjini Brasilia siku ya Jumatano.

Wakili wake , Maira Fernandes aliambia Rueters : Neymar ametoa taarifa .

”Alichukua hatua ya kuja haraka ili kutoa taarifa , ili kuweka uwazi kila kitu kilichohitajika kuwekwa wazi”.

”Tuna matumaini kwamba tutahakikisha kua mteja wetu hana hatia. Mkakati ulikuwa mrefu lakini alitoa ufafanuzi uliohitajika”.

Akizungumza katika mlango wa kituo cha polisi, Neymar alisema: Nathamini usaidizi niliopata na ujumbe wote ambao ulimwengu umenitumia, marafiki zangu, mashabiki wangu, na ulimwengu uko nami. Nataka kusema ahsante sana kwa ujumbe huo wa kunipa moyo na nahisi kwamba ninapendwa sana”.

Je anatuhumiwa na nini?

Bi Trindade ambaye pia ni raia wa Brazil anasema kuwa alikutana na Neymar katika mtandao wa Instagram.

Alikimbia chombo cha habari cha Brasil cha SBT kwamba alivutiwa na mchezaji huyo wa Brazil na alitaka kushiriki ngono naye.

Amasema kamba alisafirishwa kutoka Paris na kulipiwa hoteli na mchezaji huyo.

Video imepatikana.Je inaonyesha nini?

Kanda ya Video inaonyesha mtafaruku kati ya bi Trindade katika chumba kimoja cha hoteli-ikidaiwa kuchukuliwa na bi Trindade.

Wawili hao wanaonekana wakiwa wamelala katika kitanda ambapo baadaye mwanamke huyo anasimama na kuanza kumpiga mwanamume aliyelala kitandani ambaye anajikinga na miguu yake.

Mwanamke huyo anasema nitakupiga, unajua kwa nini kwasababu umenipiga , mtafaruku huo ukionekana kuwa mkutano wao wa pili .

Neymar amesema kuwa yeye na bi Trindade walikutana mara mbili.

Katika mahojiano hayo ya Runinga ya SBT , Bi Trindade alisema kuwa alianza kuelewa kila kitu kilichofanyika baada ya mkutano wao wa kwanza ulipokamilika na kwamba alirudi ili kuthibitisha kitendo kilichofanyika huku akitaka haki kufanyika.

Kanda hiyo ya Video ilionyeshwa katika kituo hicho cha Brazil.

Je Neymar amesema nini?

Neymar hajatoa tamko lolote kufikia sasa kuhusu mahojiano hayo ya runinga.

Babake Neymar dos Santos , alihojiwa na TV Record kuhusu kanda hiyo ya video iliochukuliwa katika chumba cha hoteli na alisema kuwa ,mwanawe alikuwa ametegwa na kwamba Neymar alikuwa hana hatia.

Katika taarifa ya mapema , Usimamizi wa Neymar uliziita shutuma hizo kuwa zisizo na haki na kusema kuwa mchezaji huyo alikua mwathiriwa wa jaribio la kumlaghai. Neymar alirudia madai hayo ya ulaghai katika ukurasa wake wa Instagram kwa dakiika saba.

Akizungumza kwa lugha ya Kireno , mchezaji huyo alisema: Kile kilichotokea siku ile ni mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamume na mwanamke ndani ya chumba kama inavyokuwa kati ya wapenzi wawili.

Na siku iliofuatia hakuna kubwa lililotokea. Tuliendelea kutumiana ujumbe . Aliniomba zawadi ya mtoto wake .

Katika kanda hiyo ya video , mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alionyesha kile alichokitaja kuwa msururu wa ujumbe wa WhatsApp kati yake na Trindade , ikiwemo picha za kimapenzi naye.”

Anasema kwamba alilazimika kuziweka wazi ili kuonyesha kwamba kulikuwa hakuna na mno. katika mahojiano hayo bi Trindade alikana kujaribu kumlaghai bi Trindade akisema kuwa . Nataka haki na sio kulipwa fidia ya kifedha.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro alimtembelea Neymar hospitalini baada ya mchezaji huyo wa kandanda kupata jeraha siku ya Jumatano ”akimtakia kupona kwa haraka” ,bwana Bolsonaro alisema awali.

”Yuko katika hali ngumu lakini namuamini”.

Je hali ya kisheria ikoje?

Mawakili waliomwakilisha bi Trindade wanasema kuwa malalamishi yake ya kwanza yalikuwa ya uchokozi ama kupigwa na Neymar.

Wanasema kwamba walikuwa wamekubaliana jinsi ya kutatau swala hilo na mawakili wa Neymar lakini baadaye mawakili hao walikataa.

Mawakili wa pande zote mbili walitofautiana kuhusu ni nani haswa aliyeitisha kikao hicho.

Baadaye Trindade aliwasilisha mahakamani madai yake siku ya Ijumaa mjini Sao Paulo.

Neymar pia huenda akakabiliwa na uchunguzi kuhusu kuchapisha picha za Trindade bila ruhusa yake ka kuwa kitendo hicho huenda kikakiuka sheria za kulinda faragha ya mtu.

error: Content is protected !!