Ndege kubwa kupata kutengenezwa yajaribiwa

Ndege kubwa kabisa kupata kutengenezwa duniani yaruka kwa mara ya kwanza.

Ndege hiyo ijulikanayo kwa jina la “Roc” imetengenezwa na shirika la urushaji roketi Strato launch. Ndege hiyo ina uzito wa tani 226 na mbawa za ukubwa wa mita 117.

Ndege hiyo iliruka kwa mara ya kwanza katika safari yake ya majaribio katika uwanja wa ndege wa Mojave katika jimbo la Kalifornia.

Shirika la Strato launch limesambaza picha za video zinazoonyesha ndege hiyo ikiruka katika safari yake ya majaribio. Ndege hiyo ina Injini 6  za Boing 747 na miili miwili.

Safari hiyo ilidumu kwa muda wa dakika 150 na kisha ndege hiyo ilitua salama. Mkurugenzi mkuu wa shirika la Strato launch Jean Floyd alisema kwamba kwake yeye anapata hisia za ajabu anapoona ndege hiyo inaruka.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani 250 ambayo imebuniwa ili itumike katika tafiti za masuala ya anga. Ndege hiyo itabeba roketi kuelekea angani umbali wa kilomita 10, na kutokea hapo ndipo roketi zitarushwa , hilo litaongeza ufanisi katika kurusha sateliti zikae kwenye obit zake.

error: Content is protected !!