Nafasi za Kazi

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 2011.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inatangaza nafasi za Kazi katika maeneo yaliyoainishwa hapo chini, kwa wazanzibar wenye sifa zinazohitajika.

1. KATIBU MUKHTASI DARAJA LA III (Nafasi 1 Unguja)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar
* Awe amehitimu Stashahada ya fani ya Uhazili kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu

* Kusaidia kupiga chapa taarifa za siri, madokezo, taarifa na nyaraka nyengine
* Kusaidia kutunza taarifa, kumbukumbu za matukio mbali mbali.
* Kupokea na kupeleka faksi.
* Kusaidia kupokea na kuwakaribisha wageni wa ofisi.
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake.

2. AFISA UHUSIANO DARAJA II ( Nafasi 1 Unguja )

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar.
* Awe amehitimu Shahada ya Kwanza /Stashahada ya Juu au Stashahada ya Uzamili katika fani ya Uhusiano wa Kimataifa/Uandishi wa Habari/Uhusiano wa Umma (Public Relation) au fani inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu

* Kushiriki katika utayarishaji wa vipeperushi na matangazo ya kuitangaza Mamlaka.
* Kupokea malalamiko kwa wadau na wananchi kwa ujumla juu ya utendaji wa Mamlaka.
* Kusaidia katika Kupokea wageni wa Mamlaka.
* Kushiriki katika kuyatafutia ufumbuzi malalamiko yaliyowasilishwa.
* Kusaidia kuitangaza Mamlaka kwa kuandaa vipindi vya redio, makala katika gazeti na vipeperushi juu ya umuhimu wa shughuli zake katika kuwaunganisha wananchi na kujenga maalidili mema kwa Taifa.
* Kusaidia kuchambua na kufanya uchunguzi wa malalamiko yaliyowasilishwa.
* Kupokea wageni wa Mamlaka.
* Kuandaa na kuongoza shughuli na sherehe maalumu zinazotayarishwa na Mamlaka
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake, atakazopangiwa na mkuu wake.

3. AFISA GHALA DARAJA LA II (nafasi 1 Unguja)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibari
* Awe amehitimu shahada ya kwanza/stashahada ya juu au stashahada ya uzamili ya utunzaji vifaa (Materials management) au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Majukumu

* Kufungua na kutunza ‘Bin Card’
* Kutunza ghala la vifaa
* Kutoa na kutunza stakabadhi ya kutolea vifaa katika ghala
* Kujaza na kutunza buku la kuhifadhia vifaa (ledger book)
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake.

4. MHUDUMU WA USAFI II (nafasi 6 Unguja)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar
* Awe amehitimu cheti cha kidatu cha nne na kufaulu kutoka katika mamlaka inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Majukumu

* Kusafisha mazingira yanayoizunguka majengo ya Mamlaka.
* Kutayarisha huduma za chai.
* Kuweka vifaa panapohusika.
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake, atakazopangiwa na mkuu wake.

5. MUEGESHA NDEGE MSAIDIZI DARAJA LA III (Nafasi 2 Pemba)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar
* Awe amehitimu Stashahada kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
* Mwenywe na taaluma ya Uegeshaji Ndege (Apron Management) /Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege (BAOC) na kupata leseni kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali. atapewa kipaumbele.

Majukumu

* Kusaidia kutoa taarifa za kiufundi zinazohusiana na maegesho ya ndege.
* Kusaidia kumuelekeza rubani kuegesha ndege katika maegesho yaliyosalama.
* Kushiriki katika kuweka kumbukumbu za matukio yanayoweza kusababisha ajali au matukio ya ajali yanayotokea wakati wa kuegesha ndege.
* Kusaidia kupanga nafasi za maegesho ya ndege kulingana na kanuni za uegeshaji ndege.
* Kusaidia kufanya ukaguzi wa eneo la maegesho ya ndege na kuweka kumbukumbu katika fomu za ukaguzi.
* Kuhakikisha kuwa watumiaji wote wa eneo la maegesho wanafuata taratibu za eneo hilo.
* Kufanya kazi nyengine yoyote kama atakavyoagizwa kwa mujibu wa taratibu na miongozo kutoka kwa mkuu wako wa kazi.

6. a) Fundi Sanifu Barafu (Nafasi 1 Pemba)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar
* Awe amehitimu cheti katika fani ya Barafu au fani nyengine inayolinga kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu

* Kushiriki kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa viyoyozi ili kubaini matatizo na kuyatafutia ufumbuzi.
* Kushiriki katika kutengeneza mashine zilizoharibika.
* Kushiriki kutunza usalama wa vifaa na viyoyozi katika sehemu inayohusika.
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake, atakazopangiwa na mkuu wake.

7. FUNDI MCHUNDO UJENZI (Nafasi 1 Pemba na Nafasi 1 Unguja)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar
* Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ujenzi au fani nyengine inayolingana nazo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu

* Kusaidia kusimamiana kushauri katika ujenzi wa miradi ya majengo unaofanywa na wakandarasi wadogo wadogo.
* Kusaidia katika kusimamia na kushauri mafundi wa vikundi kazi vinavyo karabati Majengo ya Mamlaka.
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake, atakazopangiwa na mkuu wake.

8. FUNDI SANIFU MAJENGO DARAJALA III (Nafas 1 Pemba na Nafasi 1 Unguja)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibari
* Awe amehitimu cheti katika fani ya Ujenzi au fani nyengine inayolinga kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu

* Kushiriki katika kusimamia ujenzi wa miradi ya majengo unaofanywa na wakandarasi wadogo wadogo.
* Kushiriki katika kusimamia mafundi wa vikundikazi vinavyokarabati Majengo ya Mamlaka.
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake.

9. FUNDI SANIFU MITAMBO DARAJALA III (Nafasi 1 Pemba)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar
* Awe amehitimu cheti katika fani ya Mitambo au fani nyengine inayolinga kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Majukumu

* Kushiriki katika kufanya ukaguzi wa ubora wa mitambo na kuirekebisha ipasavyo.
* Kushiriki katika upimaji wa mitambo kufuatana na maelekezo ya mhandisi.
* Kushiriki katika kufunga mitambo mipya ya Mamlaka.
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake, atakazopangiwa na mkuu wake.

10. FUNDI SANIFU BOMBA DARAJA LA III (Nafasi 1 Pemba)

Sifa za Muombaji

* Awe Mzanzibar
* Awe amehitimu cheti katika fani ya Mitambo au fani nyengine inayolinga kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Majukumu

* Kushiriki katika kufanya ukaguzi wa ubora wa mabomba na kuirekebisha ipasavyo.
* Kushiriki katika utengenezaji wa miundombinu mipya ya mabomba ya Mamlaka.
* Kushiriki katika kufunga mitambo mipya ya Mamlaka.
* Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake, atakazopangiwa na mkuu wake.

Jinsi ya Kuomba

Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
S.L.P 4742
Zanzibar.

Muombaji anaweza kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi za Mamlaka ya Viwanya vya Ndege Unguja / Pemba wakati wa saa za kazi. Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

a) Maelezo binafsi ya muombaji (CV)
b) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
c) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
d) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
e) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
f) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 16 Januari, 2019 wakati wa saa za kazi.

ANGALIZO

Maelezo Zaid Ya Kuhusiana Na Tangazo Hili Unaweza Kupata Katika Ofisi Ya Mamlaka Ya Viwanja Vya Ndege iliyopo kisauni

error: Content is protected !!