Mzaha wa rais wa Ufilipino kuhusu bangi wazua mjadala

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amezua mjadala baada ya kusema kwamba inabidi utumie bangi ili usisinzie kwenye vikao vinavyochukua siku nzima.

Rais huyo mwenye miaka 73 aliyasmea hayo kwenye sherehe za utoaji zawadi za jumuia ya Umoja wa nchi za kusini mwa Asia (ASEAN) mwezi uliopita nchini Singapur.

Ni mara kadhaa rais huyo amekuwa akitoa kauli bila kufikiria na baadae zimekuwa zikizua mijadala, mara tu baada ya kutoa kauli hiyo rais huyo alisema anatania.

Nchini Ufilipino katika utawala wa Duterte watu wapatao elfu 5 wameuawa na vyombo vya usalama kwa kuzaniwa wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Katika kupiga vita biashara haramu ya madawa ya kulevya Duterte alitoa amri kwamba yeyote atakayejihusisha na biashara hiyo hata kama akizaniwa tu auawe.

Makundi mbalimbali ya haki za binadamu nchini Ufilipino na Ulimwenguni kwa ujumla yamekuwa yakimpinga kwa nguvu sote kutokana na amri hiyo kwa kigezo kwamba ni kinyume cha haki za binadamu.

error: Content is protected !!