Mtoto wa Sheikh Zakzaky: Hali ya kimwili na kiafya ya baba yangu ni mbaya

Mwana wa Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria ametahadharisha kupitia ujumbe aliotoa kwamba hali ya kimwili ya baba yake ni mbaya sana. Amesema karibu njia zote zimeshindikana kwa ajili ya kunusuru maisha yake.

Muhammad Ibrahim Zakzaky ameeleza kuwa kuna mada nyingi za sumu ya risasi na cadmium kwenye damu ya baba yake na kwamba serikali ya Nigeria haijachukua hatua yoyote ya kumfikisha hospitali Sheikh Zakzaky ili alazwe kwa ajili ya matibabu. Hali ya kiongozi huyo wa Waislamu hivi sasa ni mbaya ikiwa imepita miaka mitatu na nusu tangu kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria afungwe jela kinyume sheria na kutoachiwa huru licha mahakama nchini humo kuamuru aachiwe huru. 

Chunguzi mpya za kitiba zimethibitisha kuwa katika damu ya Sheikh Zakzaky kuna mada za sumu ya risasi na cadmium; jambo linaloonyesha kuwa sumu hiyo alipewa akiwa jela. Harakati ya Kiislamu ya Nigeria kwa mara nyingine tena imetaka kuachiwa huru Sheikh Zakzaky na mkewe kufuatia kuzidi kuwa mbaya hali ya kiafya na kiongozi huyo wa Waislamu na mkewe. Hata hivyo Mahakama Kuu katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria haijakubali kuwaachia huru watu hao tajwa.

error: Content is protected !!