Misikiti ya Makka na Madina tayari kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Misikiti mikuu ya Makka na Madina nchini Saudia yaanza maandalizi kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika maandalizi hayo mazulia yote katika misikiti hiyo yamebadilishwa. Ukurasa wa Wizara inayoshughulika na  misikiti ya Makka na Madina umeandika kwamba mazulia yote katika misikiti hiyo miwili yamebadilishwa na kuwekwa mapya.

Habari hiyo imeripoti kwamba mazulia elfu 21 yamebadilishwa katika msikiti wa Makka huku katika msikiti wa Madina mazulia elfu 3 yamebadilishwa. Taarifa hiyo imefahamisha kwamba ili kuwezesha waumini zaidi kufanya ibada katika misikiti hiyo, eneo la ziada limeongezwa katika misikiti hiyo.

Waislamu kote ulimwenguni wanataraji kuanza kufunga mwezi wa Ramadhani kati ya Mei 6 hadi 8 kutegemea na mwandamo wa mwezi.

error: Content is protected !!