Messi 45, Ronaldo 44, mchaka mchaka wa mwaka

Messi na Ronaldo ni Wanasoka machachari ambao wameutingisha ulimwengu wa soka kwa zaidi ya Muongo mmoja sasa.

Nyota hao wawili wamechukua tuzo 10 za Ballon D’Or yani mwanasoka bora wa mwaka huku kila mmoja akichukua mara 5. Ukiachilia mbali hilo, Messi na Ronaldo pia wamekua katika ubora wa hali ya juu wakinyaka medali mbalimbali katika vilabu vyao kama vile ubingwa wa Ulaya, ubingwa wa kombe la mfalme na kombe la Ligi kuu nchini Hispania.

Mwaka huu umekua ni mwaka mwingine wa mafanikio kwa nyota hao wawili ambapo Messi mpaka sasa ameweza kufunga jumla ya magoli 45 ndani ya mwaka huu Huku ronaldo akimfuatia kwa magoli 44.

Mwezi mmoja uliosalia kuumaliza mwaka unaonekana kuwa wa kuvutia na kutingisha sana ukizingatia kwamba wote watakua mbioni kuisaka tuzo hiyo.

Robert Lewandowsky ndiye mchezaji anayewafuatia kwa karibu akiwa na magoli 41 ndani ya mwaka huu.

Tuzo hiyo ilichukuliwa na nyota wa Tottenham na Uingereza, Harry kane hapo mwaka jana.

Je ni Messi au Ronaldo atakayeibuka mbabe kwa mwaka huu ?

error: Content is protected !!