Mchafuko ya kibiashara baina ya China na Marekani unavyoshika kasi

Itakapohitajika shirika la vifaa vya kielektroniki la Apple litazalisha bidhaa zake nje ya China.

Kwa mujibu wa habari kutoka katika tovuti ya Bloomberg, Young Liu, mmoja wa wakurugenzi wa shirika la Hon Hai lenye makao makuu yake Taiwan lijulikanalo pia kama “Foxconn” mshirika muhimu wa Apple katika uzalishaji amesema kama vita ya kibiashara baina ya Marekani na China itaendelea kushika kasi wao wataiunga mkono Apple kikamilifu.

Liu alisema mpaka hivi sasa asilimia 25 ya uzalishaji unafanyika nje ya China na kwamba India pia imewekeza katika Apple. Aliongeza kwamba Apple inao uwezo wa kutosha kushibisha mahitaji ya soko.

Liu alisema Apple bado haijawapa maagizo ya kuhama China, lakini shirika lina uwezo wa kuhamishia uzalishaji sehemu yeyote kwa kuzingatia mahitaji ya wateja.

Hivi sasa Shirika la Foxconn linafanyia majaribio ya ubora toleo la iPhone Xr  katika mji wa Chennai nchini India, ndani ya muda mfupi toleo hilo  limepangwa kuanza kuzalishwa.

Ili kuziba pengo la kibiashara ya kimataifa Marekani ilianza kwa kuongeza tozo la forodha kwa bidhaa za aluminium na paneli za jua zinazoagizwa kutoka China mnamo mwezi Machi mwaka 2018. China nayo ilijibu mapigo kwa kuongeza kodi kwa bidhaa kutoka Marekani na hapo ndipo vita ya kibiashara na mchafukoge yote ilipoanza kushika kasi baina ya China na Marekani.

Kuzuiwa kwa Huawei kutumia Android kikamilifu kumepelekea mataifa hayo makubwa kuanza kushambuliana katika upande wa teknolojia.

error: Content is protected !!