Marekani yatwaa kombe la dunia

Marekani imetwaa kombe la dunia la FIFA wanawake 2019  baada ya kuilaza Uholanzi mgoli 2-0.

Mashindano ya kombe la dunia ya wanawake yaliyokuwa yakifanyika nchini Ufaransa ni mashindano ya 8 kuandaliwa. Katika fainali Marekani ilikutana na Uholanzi.

Kipindi cha kwanza kilimalizika bila magoli, Mnamo dk 61, Megan Anna Rapinoe, aliipatia goli la kwanza Marekani kwa mkwaju wa penati. Dk ya 69 Rose Lavelle aliipatia Marekani goli la 2.

Hii ni mara ya nne kwa Marekani kutwaa kombe hilo. Marekani ilitwaa kombe hilo 1991,1999 na 2015.

Katika mashindano hayo Marekani ilishinda michezo yote 7 iliyocheza ikipachika magoli 26 na kuruhusu magoli 3 pekee.

error: Content is protected !!