Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA Yatangaza Bei Mpya ya Mafuta Zanzibar Kuazia leo 10/7/2019.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imefanya mabadiliko ya bei za mafuta ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia leo 10/07/2019.

Akitoa taarifa hiyo jana kwa vyombo vya habari Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ( ZURA) Khuzaimat Bakari amesema kuwa bei za mafuta kwa mwezi wa Julai zimeshuka kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, gharama za usafirishaji pamoja na bima.

Amesema kuwa bei mpya ya mafuta ya Petroli sh.2,338 ambayo sawa na asilimia 1.59%, mafuta ya dizeli yatauzwa kwa bei sh.2,319 sawa na asilimia 0.42%.

Aidha amesema kuwa bei mpya ya mafuta ya taa ni sh.1,753 sawa na asilimia 0.075% na mafuta ya Banka yameshuka na itakuwa ni sh.2.145 sawa na asilimia 0.46%.

Hata hivyo Khuzaimat amesema kuwa bei hiyo ni halali ambazo zitaanza kutumika hapo leo.

error: Content is protected !!