Liverpool watwaa ubingwa wa Klabu bingwa barani Ulaya

Majogoo wa soka wa Uingereza, Liverpool hapo jana wameibuka kidedea katika fainali ya klabu bingwa balani Ulaya dhidi ya Tottenham.

Liverpool wanaupata ushindi huo ikiwa ni mwaka mmoja tangu walipochakazwa na Real Madrid katika fainali ya msimu uliopita. 

Tangu dakika ya kwanza ya mchezo, kijana Mjerumani, Jugen Klopp alionekana kuwa mwiba mkali dhidi ya Tottenham Hotspurs ya jinini London. Mnamo dakika ya pili, mshambuliaji wao nyota Mohamed Salah alifanikiwa kuiweka mbele Liverpool kwa kuifungia goli la kwanza kwa Mkwaju wa penalti kufuati mpira ulioshikwa na Moussa Sissoko. 

Goli hilo la nyota huyo wa Misri lilidumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza na timu zote zikaelekea mapumzikoni. Linakua ni goli la pili kufungwa kwa haraka Zaidi katika fainali hizo huku la kwanza likiwa ni lile la Paolo Maldini alilofunga dhidi ya Liverpool mwaka 2005.  

Kipindi cha pili, Klopp alifanya mabadiliko ya kikosi chake na kumtoa Mbrazil Robberto Firmino, maarufu kama Boby na kumuingiza Origi. Mabadiliko hayo yalizaa matunda ambapo mnamo dakika ya 86 ya mchezo, Origi aliipatia bao la pili liverpool na kuifanya mechi hiyo kufika mwisho. 

Hadi kipenga cha mwisho, Liverpool waliibuka kidedea kwa magoli 2 kwa bila. 

Hii ni mara ya Sita kwa timu ya soka ya Liverpool kutwaa taji hilo maarufu zaidi barani Ulaya. Liverpool walilikosa kombe la ligi kuu baada ya kupitwa alama moja na waliokua mahasimu wao wakuu kwenye ligi hiyo, Manchester City. Liverpool ilimaliza ikiwa na alama 97 huku Man City wakiwa na alama 98

error: Content is protected !!