Kamisheni ya Umoja wa Afrika yaunga mkono juhudi za kutatua hitilafu za Eritrea-Ethiopia

Kamisheni ya Umoja wa Afrika yaunga mkono juhudi za kutatua hitilafu za Eritrea-Ethiopia

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amepongeza juhudi zilizofanyika kwa ajili ya kuondoa hitilafu baina ya nchi mbili za Ethiopia na Eritrea.

Moussa Faki Mahamat amesema kuwa Kamisheni ya Afrika inapongeza mchakato wa kutatua hitilafu baina ya nchi za Ethiopia na Eritrea na kwamba AU inakaribisha mafanikio ya hivi karibuni katika eneo la Pembe ya Afrika.

Tarehe 16 mwezi Julai Rais Isaias Afewerki wa Eritrea alifungua ubalozi wa nchi yake mjini Addis Ababa baada ya uhusiano wa nchi hizo mbili kukatwa kwa kipindi cha miaka 20.

Tarehe 19 mwezi huo huo Ethiopia ilimteua Ridhwan Hussein kuwa balozi wake nchini Eritrea.

Viongozi wa Eritrea na Ethiopia.

Nchi hizo mbili za Eritrea na Ethiopia hivi karibuni zilihitimisha rasmi vita baina yao ambavyo vinatambuliwa kuwa mapigano ya muda mrefu zaidi ya kijeshi barani Afrika. Karibu watu elfu 80 waliuawa katika vita hivyo.

Eritrea ilijitenga na Ethiopia mwaka 1993 baada ya mapigano ya muda mrefu ya kutaka kujitawala. Hitilafu za kugombania maeneo ya mpakani hapo mwaka 1998 zilisababisha vita vikubwa baina ya pande hizi mbili vilivyoendelea kwa kipindi cha miaka miwili na kuua makumi ya maelfu ya watu.

error: Content is protected !!