John Kerry: Trump amethibitisha kivitendo maneno ya wapinzani wa JCPOA ndani ya Iran

John Kerry, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani kwa mara nyingine tena amekosoa misimamo ya serikali ya rais wa hivi sasa wa nchi hiyo Donald Trump dhidi ya Iran na kuionya Ikulu ya nchi hiyo White House kuhusu matokeo mabaya ya siasa hizo.

John Kerry amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya CNN na huku akisema kuwa siasa za Trump ni hatari kwa Marekani amesema, Donald Trump amethibitisha ukweli wa maneno ya watu wanaosema kuwa Marekani si nchi ya kuiamini.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa serikali ya zamani ya Marekani ambaye serikali yake ndiyo muhusika mkuu wa mapatano ya nyuklia na Iran amemlaumu Trump kwa kujitoa katika mapatano hayo na kusema kuwa hatua hiyo imechukuliwa bila ya kutegemea stratijia yoyote ya maana.

Rais wa Marekani, Donald Trump amejitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA bila ya hata kusoma kilichoandikwa ndani yake

 

Kabla ya hapo pia, John Kerry alimlaumu vikali Trump kwa siasa zake dhidi ya Iran na dhidi ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Itakumbukuwa kuwa tarehe 8 Mei mwaka huu, Donald Trump alitangaza kuitoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kurejesha vikwazo vyote vya Marekani dhidi ya Iran.

Hadi hivi sasa Trump analaumiwa kimataifa kwa uamuzi wake huo wa kiuanagenzi na wa kiuadui. Kwa hatua yake hiyo, Trump amezidi kuithibitishia ulimwengu kuwa Marekani si nchi ya kuiamini hata kidogo.

Pande nyingine zilizofanikisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA na Iran yaani Uingereza, Ufaransa, Ujerumaini, Russia, China na Umoja wa Ulaya zimesema zitaendelea kuheshimu mapatano hayo na hivyo kuifanya Marekani itengwe kimataifa.

error: Content is protected !!