Je Serikali zinafanikiwa vipi kuibana huduma za Internet?

Ndilo jambo linalozidi kuwa la kawaida katika baadhi ya mataifa ya Afrika, ambako serkali zimezima mara kwa mara inteneti au kuzuia mitandao ya kijamii.

Ni mwaka mmoja tangu Chad kubana mitandao maarufu ya kijamii na miezi kadhaa baada ya mawasiliano ya intaneti kufungwa katika miji muhimu ya taifa la DR Congo baada ya uchaguzi mkuu.

Sudan ilibana nafasi ya raia kuingia katika mitandao wakati wa maandamano dhidi ya serikali kama ilivyokuwa nchini Zimbabwe.

Wanaharakati wa dijitali kutetea haki wanasema ni kubana taarifa, lakini serikali zinadai inasaidia kuimarisha usalama.

Basi serikali inafanikiwa vipi kufunga au kubana mitandao?

Kubana uwezo wa kuingia

Serikali inaweza kubana matumizi ya intaneti kwa kuagiza makampuni yanayotoa huduma za intaneti (ISPs) kudhibiti au kubana uwezo wa wateja kuingia katika mitandao.

Mara nyingi huwa kuna kizuizi kinachowekwa kwa wateja kutofika katika mitandao ya kijamii yanayotumika kwa sana.

Kwa hatua kali zaidi, serikali inaweza kuagiza kufungwa kabisa huduma nzima ya intaneti.

Mnamo 2018, kulikuwa na visa 21 ambapo intaneti ilifungwa kwa kiwango fulani au kabisa, ikilinganishwa na visa 13 mnamo 2017 na visa 4 mnamo mwaka 2016, kwa mujibu wa kundi la uangalizi la kujitegemea Access Now.

Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Chad, Cameroon, Sudan, Ethiopia, Mali, Nigeria na Sierra Leone zilibana intaneti mwaka jana.

Ni mtindo unaodhihirika dunani. Mnamo 2018, kulikuwana visa 188 vya intaneti kubanwa ikilinganishwa na 108 mnamo 2017 na 75 mnamo 2016.

Katika kila nchi, ni umauzi wa makampuni yanayotoa huduma hiyo ya intaneti kutekeleza maagizo ya serikali kubana intaneti.

Mfumo mmoja unaotumika unafahamika kama URL-based blocking. Huu ni mfumo unaohusisha kuweka kizuizi kinacho zuia wateja kuingia katika mitandao iliyo pigwa marufuku.

Mteja anayejaribu kuingia katika mitandao hiyo hupata ujumbe “server not found” au mtandao haupatikani – umezuia na msimamizi wa mtandao.

Mfumo mwingine unafahamika kama ‘throttling’.

Mbinu hii huzuia kwa kiwango kikubwa idadi ya wateja wanaotembelea mtandao maalum, na kutoa hisia kwamba kasi ya huduma ni ndogo na kuwafanya wateja waelekee kwingine.

Hili ni la afueni, kwasabbau ni vigumu kutambua iwapo mitandao inauia wazi au ni kutokana na mapungufu ya miundombinu duni.

Kama hatua ya mwisho, makampuni ya mawasiliano yanaweza kutakiwa kufunga kabisa huduma kwa ujumla na kuzuia wateja kupokea data yoyote.

Ja makampuni ya kutoa huduma yanaweza kusema Hapana?

Uwezo wa serikali kubana intaneti unategemea uwezo wao kudhibiti makampuni ya mawasiliano nchini.

Makampuni ya kutoa huduma ya mawasiliano yanapewa vibali na serikali, jambo linalomaanisha kwamba huenda wakatozwa faini au wakapoteza mikataba.

Huena wateja wakawa na wahaki ya kukata rufaa mahakamani, lakini ki uhalisi ni aghalabu kuona hilo likifanyika.

mapema mwaka huu mahakama nchini Zimbabwe iliamua kurudishwa huduma ya intaneti baada ya serikali kuagiza ibanwe.

Kwa upande wake serikali ya Zimbabwe imeidhinisha sheria mpya zinazoipatia udhibiti mkubwa katika matumizi ya intaneti.

Waziri wa habari Zimbabwe Monica Mutsvangwa anasema hili “litahakikisha kwamba intaneti na teknolojia zinazohusika zinatumika kwa manufaa ya jamii, na sio kukiuka usalama wa kitaifa.”

Lakini kuna mifano pia ambapo serikali zinazotaka kufunga intanetizinakuwa na urahisi wa kulitekeleza hilo.

“Kuna mataifa kama Ethiopia ambapo sekta ya mawasiliano ya simu bado iko chini ya serikali”, anasema Dawit Bekele, mkurugenzi wa ofisi za Afrika za jamii ya Intaneti.

Lau kama intaneti imefungwa kabisa kuna namna ambazo wateja wanaweza kutumia kuepuka vizuizi vilivyopo na kuingia katika mitandao.

Mbinu inayofahamika sana ni ya kutumia mitandao inayoruhusu kuruka vizuizi (VPNs).

mitandao hii huwa kama njia, inayofanya kuwa vigumu kwa makampuni ya kutoa huduma za intaneti kuweka vizuizi kwa mitandao iliyopigwa marufuku.

Serikali zinaweza pia kuzuia VPNs, lakini sio sana kushuhudiwa kufanya hivyo kwasababu hutatiza shughuli za wanadiplmasia na makampuni makubwa yanayotegemea intaneti kwa shughuli zao.

Baadhi ya mataifa yametaja sababu ya kusambaa kwa “habari za uongo” katikamitandao kama sababu ya kuidhinisha vikwazo hivyo.

Lakini wachambuzi na viongozi wa upinzani wanataja hii kuwa sababu ya kukandamiza makundi yanayozikosoa serikali, ambayo hutumia mitanda kama Facebook na WhatsApp kujipanga.

CHANZO: BBC

error: Content is protected !!