Israel yamwaga vitisho kwa Iran

Waziri wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa vitisho vikali kwa nchi ya Iran.

“Ndege za kivita za F-35 za Israel zina uwezo wa kufika eneo lolote mashariki ya kati ikwemo Iran  na Syria”,alisema waziri huyo.

Netanyahu ametoa vitisho hivyo kwa Iran wakati wa ziara ya Kituo cha Air Nevatim kusini mwa nchi.

Baada ya uchunguzi katika uwanja wa ndege, Netanyahu, akizungumzia ndege za kivita amesema

“Iran imesababisha maangamizi Israel, wanapaswa kukumbuka kwamba ndege hizi zinaweza kufika popote huko Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na Iran na Syria.” 

Netanyahu, ambaye mara nyingi amekuwa akiilalamikia Tehran kwa kuzalisha silaha za nyuklia, amesema kuwa Israel haitaruhusu Iran kupata silaha za nyuklia hata kwa dawa.

error: Content is protected !!