Iran imepiga marufuku shughuli na Bitcoin, fedha za crypto

Iran imepiga marufuku shughuli na Bitcoin, fedha za crypto.

Akizungumza na shirika la habari la Iran, Makamu wa Rais wa Benki Kuu,  Nasır Hakimi amesema kuwa shughuli na Bitcoin zilizuiliwa na uamuzi wa Baraza Kuu la Fedha za Kupambana na Black Market.

Nasir ambaye amewaonya watumiaji wa fedha za crypto kuhusu hatari za kuwekeza katika fedha hizo,

“Nchini Iran, Bitcoin ni marufuku kununua na kuuza .. kupanda kwa kiasi kikubwa kwa bei ya Bitcoin kumepelekea kupigwa marufuku kisheria utumiaji wa fedha hizo. Niwashauri wananchi wasiingie katika mchezo huu.” alisema.

Nasir amebainisha kuwa uzalishaji wa Bitcoin bado haujazuiliwa.

Ali Mueyyidi, Rais wa Mamlaka ya Kupambana na Uhamiaji wa Bidhaa na Fedha za Kigeni, ameviambia vyombo vya habari katika mji mkuu Tehran kwamba shughuli zote zinazohusiana na Bitcoin zimezuiliwa na wale ambao hawatokubaliana na marufuku hiyo watashughulikiwa.

Iran, ambayo ina matatizo katika biashara ya kimataifa kutokana na vikwazo vya Marekani  Umoja wa Mataifa, imeongeza kasi ya shughuli zilizofanywa kwa sarafu ya crypto.

error: Content is protected !!