Hatua kuchukuliwa dhidi ya kauli za kimadhehebu na kisiasa kipindi cha hija Saudia

Saudia  yafahamisha kuwa hatua muhimu zimechukuliwa kupiga marufuku  nyendo za aina yeyote zinazobashiri madhehebu au misimamo ya kisiasa katika kipindi cha ibada ya hija mwaka 2019.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na  kituo cha habari cha taifa cha Saudia SPA, mkutano wa shura uliofanyika  mjini Jeddah chini ya  uongozi wa mwanamfalme Mohammed Bin Salman ni kwamba hatua muhimu  zimechukuliwa kukabiliana na  nyendo ambazo zitakuwa na malengo ya kuonesha mitazamo ya kisiasa, kiadhehebu na mtazamo mingine zimechukuliwa.

Nyendo hizo zimepigwa marufuku katika ibada ya hija ambayo ni moja ya nguzo za uislamu.

Waumini katika ibada  hiyo ya hija wameombwa kuwa  wastaarabu na kuzingatia masharti ya ibada.

error: Content is protected !!