Gazeti la Washington Post: Pompeo amepuuzwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliyekuwa amefanya safari mjini Brussels hapo jana amepuuzwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Ulaya.

Gazeti la Washington Post la nchini Marekani limeandika kuwa, Pompeo aliyefanya safari ya ghafla mjini Brussels kwa lengo la kukutana na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tatu za Uingereza, Ujerumani na Ufaransa ili kujadiliana nao kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mapatano ya nyuklia ya JCPOA, alipuunzwa na viongozi hao wa Ulaya. Kwa Mujibu wa gazeti hilo, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tatu zilizotajwa za Ulaya hata hawakuwa tayari kupiga picha na Pompeo.

Hii ni katika hali ambayo awali Bi Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya alinukuliwa akisema kuwa binafsi hakuwa na ratiba yoyote kwa sasa ya kukutana na Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani mjini Brussels. Kikao cha viongozi wa nchi tatuu za Ulaya kuhusu kadhia ya mapatano ya nyuklia ya Iran JCPOA kilifanyika jana jioni kwa kuhudhuriwa na Bi Federica Mogherini na Mike Pompeo. Aidha Jumatatu ya jana Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kwamba Pompeo alibadili ghafla safari yake ya kuelekea mjini Moscow na badala yake kuelekea Brussels kwa lengo la kukutana na kuzungumza na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya juu ya Iran na mapatano hayo ya nyuklia.

error: Content is protected !!